Loading...
title : DC wa Gairo aishauri Ilala wajenge Kiwanda cha Nishati mbadala
link : DC wa Gairo aishauri Ilala wajenge Kiwanda cha Nishati mbadala
DC wa Gairo aishauri Ilala wajenge Kiwanda cha Nishati mbadala
Mwambawahabari
Mkuu wa wilaya ya Gairo (katikati)Siriel Shaidi angalia bidhaa za Wajasiliamali wa MANISPAA ya Ilala banda la ILALA Nanenane Morogoro Leo katika maonesho ya Wakulima alipotembelea banda hilo wa kwanza (kushoto) Mkuu wa Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika Estar Msome (PICHA NA HERI SHAABAN)
Na Heri Shaban, Morogoro
MKUU wa wilaya ya Gairo Siriel Shaidi ameifagilia Halmashauri ya Ilala katika viwanja vya Nanenane Morogoro alipotembelea Katika sekta ya Nishati Mbadala.
Mkuu wa wilaya Gairo aliyasema hayo Mkoani Morogoro katika banda la Manispaa ya Ilala alipotembelea upande wa sekta ya nishati mbadala kwa kutengeneza mkaa endelevu.
"Nawapongeza Ilala wamepiga hatua ni katika manispaa nilizotembea Ilala wamenivutia zaidi upande wa utengezaji nishati mbadala bila kuharibu misitu "alisema Shaidi.
Alisema atamshauri mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuzungumza na wadau wa Maendeleo kuweza kupata fedha za kununulia mashine kubwa za kutengeneza Mkaa mbadala.
Alisema Kama Serikali atamfikishia Waziri mwenye Mamlaka alichokiona Manispaa ya Ilala katika nishati mbadala ili wafanye taratibu wa kujenga kiwanda ili uzalishwe Ilala tuache Kitumia mkaa wa asili unaribu misitu na vyanzo vya maji .
Aidha alisema nishati hiyo mbadala wanatengeneza kwa kutumia mabaki ya vitu mbalimbali kwa kutengeneza mkaa salama bila kufanya uharibifu wa misitu.
Pia kwa upande Wajasiliamali wadogowadogo alisema amekutana na changamoto ya Mifuko ya vifungashio wengi wanachukua Kenya hivyo atazungumza na SIDO kwa ajili ya taratibu wa kutengeneza vifungashio.
Kwa upande wake Mtalaam wa kutengeza nishati mbadala Wema Makundi kutoka Pugu Mnadani alisema MANISPAA ya Ilala wanatengeneza mkaa salama kwa ajili ya kutunza mazingira pamoja na hifadhi ya misitu.
Wema aliwataka wananchi kutumia mkaa salama kwa Maendeleo ya viwanda.
"Changamoto kubwa iliyokuwepo garama ya mashine ndogo shilingi milioni 15 mashine kubwa milioni 40 ya kutengeneza mkaa tunaomba Serikali itusaidie vitendea kazi ili manispaa ya Ilala tuweze kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitasambaza mkaa nchi nzima
Hivyo makala DC wa Gairo aishauri Ilala wajenge Kiwanda cha Nishati mbadala
yaani makala yote DC wa Gairo aishauri Ilala wajenge Kiwanda cha Nishati mbadala Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC wa Gairo aishauri Ilala wajenge Kiwanda cha Nishati mbadala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/dc-wa-gairo-aishauri-ilala-wajenge.html
0 Response to "DC wa Gairo aishauri Ilala wajenge Kiwanda cha Nishati mbadala"
Post a Comment