Loading...
title : FM ACADEMIA KUTOA BURUDANI SEPTEMBA 1 KATIKA UKUMBI WA FILOMENA MKOANI KILIMANJARO
link : FM ACADEMIA KUTOA BURUDANI SEPTEMBA 1 KATIKA UKUMBI WA FILOMENA MKOANI KILIMANJARO
FM ACADEMIA KUTOA BURUDANI SEPTEMBA 1 KATIKA UKUMBI WA FILOMENA MKOANI KILIMANJARO
Na Woinde Shizza, Kilimanjaro
BENDI ya FM Academia ya jijini Dar es Salam imeahidi kutoa burudani ya nguvu Septemba moja katika ukumbi wa Filomena Klabu uliopo Hai mkoani kilimanjaro.
Akizungumza na waandishi wa habari Kiongozi wa bendi hiyo Pacho Mwamba amesema bendi hiyo ikiwa chini yake itaangusha burudani ya nguvu katika usiku wa kuazimisha miaka minne ya tangu kuanzishwa kwa Bendi ya Filomena Pamoja na ukumbi wa sherehe na klabu ya Filomena tangu ianzishwe.
Amefafanua kuwa wamejipanga vizuri kwa ajili ya kuwapa burudani wakazi wa moshi Pamoja na vitongoji vyao huku wakibainisha kuwa siku hiyo watatumia pia kuwatambulisha wimbo wao wa Rivasi nakuwaonyesha wakazi wa kilimanjaro na vitongoji vyake jinsi unavyochezwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Filomena band na klabu Swaumu Kileo amewaambia waandishi wa habari kuwa onesho hilo litafanyika Septemba 1.
Amesema mbali na FM Academia kutoa burudani siku hiyo pia kutakuwa na burudani zingine za aina mbalimbali zitakazo tangulia kabla ya bendi ya nyumbani pamoja na Fm Academia kupanda jukwaani majira ya sa a mbili usiku. Amesema kama ilivyo kawaida ya Filomena kuwapa burudani watu wa mkoani kilimanjaro, hivyo hivyo wataendelea kuwapa burudani wananchi wote ikiwa ni desturi yao
Saumu ametaja viingilio vya siku hiyo kuwa kwa viti maalumu(V.I.P)ni Sh.10, 000 na kawaida huku kawaida ikiwa ni Sh. 7000 tu.
Ametoa rai kwa wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani kufika siku hiyo kwani kuna mambo mazuri wameyaandaa kwa ajili yao na kubwa zaidi ni siku ambayo wanasheherekea miaka minne tangu ilipoanzishwa bendi na klabu ya Filomena.
Baadhi ya Wacheza shoo wa bendi hiyo
Hivyo makala FM ACADEMIA KUTOA BURUDANI SEPTEMBA 1 KATIKA UKUMBI WA FILOMENA MKOANI KILIMANJARO
yaani makala yote FM ACADEMIA KUTOA BURUDANI SEPTEMBA 1 KATIKA UKUMBI WA FILOMENA MKOANI KILIMANJARO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala FM ACADEMIA KUTOA BURUDANI SEPTEMBA 1 KATIKA UKUMBI WA FILOMENA MKOANI KILIMANJARO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/fm-academia-kutoa-burudani-septemba-1.html
0 Response to "FM ACADEMIA KUTOA BURUDANI SEPTEMBA 1 KATIKA UKUMBI WA FILOMENA MKOANI KILIMANJARO"
Post a Comment