Loading...

KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA

Loading...
KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA
link : KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA

soma pia


KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA

Katika kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ubalozi wa Tanzania Seoul kwa kushirikiana na “Korea-Africa Foundation” na “Korea Chamber of Commerce and Industry” uliandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kwa wadau wa sekta ya Afya lililofanyika Seoul, Jamhuri ya Korea. Kongamano hilo la aina yake, lilijumuisha Wizara na Taasisi za kuitendaji katika eneo husika ambazo ni: Wizara ya Afya; Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Kituo cha Uwekezaji (TIC); MSD; TFDA, na TAPI (Tanzania Association Pharmaceutical Industries).

Aidha, Kongamano hilo lililolenga kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya madawa na vifaa tiba nchini Tanzania, lilihudhuriwa pia na makampuni zaidi ya 100, kutoka pande zote mbili ikijumuisha: Makampuni ya utengenezaji madawa na vifaa tiba; Vyuo Vikuu; Taasisi za utafiti; Hospitali; Vyama vya watengenezaji wa madawa na vifaa tiba; Makampuni kutoka katika sekta binafsi; na Diaspora wetu waliopo Seoul.

Katika Kongamano hilo, mada mbalimbali ziliwasilishwa zikijumuisha: Fursa zilizopo Tanzania katika sekta ya utengenezaji wa madawa na vifaa tiba, mazingira ya ufanyaji biashara na vivutio “incentives” vinavyotolewa na Serikali; Hali ya soko na uhitaji (Market Potentiality); Taratibu za kufuatwa katika uingizwaji wa bidhaa za madawa na uanzishwaji wa viwanda husika; na utayari wa sekta binafsi katika kushirikiana na wenzao wa Korea katika biashara na ubia katika viwanda vya madawa na vifaa tiba. Upande wa Korea pia ukiwakilishwa na Vyama vya watengenezaji wa madawa na vifaa tiba walitoa mada iliyokuwa na lengo la kubadilishana uzoefu na upande wa Tanzania. Kongamano lilihitimishwa kwa B2B, ambapo makampuni na Taasisi zilikutana kujadiliana zaidi fursa, maeneo ya ushirikiano, na kupata ufafanuzi wa kina katika maeneo mbalimbali; na baadaye kutembelea Makampuni ya Madawa.
Mgeni Rasmi katika Kongamano la kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya madawa na vifaa tiba, Bw. Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) akitoa Hotuba ya Ufunguzi, kwa niaba ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka akitoa neno la ukaribisho katika Kongamano hilo.
Rais wa “Korea-Africa Foundation” waandaaji wenza wa Kongamano hilo, Balozi CHOI, Yeon-ho, akitoa neno katika hafla ya ufunguzi.
Sehemu ya washiriki katika Kongamano la kuhamasisha wawekezaji wa viwanda vya Madawa na vifaa tiba Seoul, Jamhuri ya Korea, August 13, 2018.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Hivyo makala KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA

yaani makala yote KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/kongamano-la-biashara-na-uwekezaji.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA"

Post a Comment

Loading...