Loading...

LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA

Loading...
LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA
link : LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA

soma pia


LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuuliza maswali Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara mjini, Ibrahim Mhando (kushoto) baada ya kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye ni mshauri mkuu wa ujenzi wa Ofisi Kuu ya Uhamiaji Mkoani Mtwara. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mkondya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitoka Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara mara baada ya kumsweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi hicho ambaye aliwaweka watuhumiwa chumba cha upelelezi badala ya mahabusu kituoni hapo. Nyuma ya Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mkondya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuangalia Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Ujenzi ya Lucas, ambaye pia kandarasi aliyejenga Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Theophilius Kessy, wakati alipokua anambana maswali ya kutaka kujua kwanini Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara limejengwa chini ya kiwango. Aliyeshika kitabu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
                                                                                                                         
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye alitoa taarifa ya uongo kwa Waziri huyo kuhusu ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji Mkoani humo.

Tukio hilo lilitokea saa 12:46 asubuhi Agosti 27 leo Jumatatu, wakati Waziri Lugola na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Meja Jenerali, Jacob Kingu walipofika Kituo hicho kikuu cha mkoa kwa kushtukiza wakati alipokua anakwenda Uwanja wa Ndege kwa ajili ya kurudi jijini Dar es Salaam, ndipo Waziri huyo alitaka kuthibitisha kama mtuhumiwa ambaye alielekeza jana usiku akamatwe awekwe mahabusu endapo Polisi walitekeleza agizo lake.

Hata hivyo, Waziri Lugola alimkuta mtuhumiwa huyo, Benjamin Kasiga akiwa chumba cha upelelezi badala ya kuwekwa mahabusu ya polisi hiyo, ndipo akamuuliza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Lucas Mkondya, kwanini agizo lake halijatekelezwa.

“Hivi ndivyo polisi mnafanya hivi, haya ndio madudu mnayoyafanya? Tabia hii siku zote tunaipinga ikichafua Jeshi la Polisi, na hii ndiyo tabia yenu, najua ndio mana nimekuja ghafla, mnafahamu maadili ya Jeshi? RPC hawa polisi wako wanafanya nini, OCS njoo hapa, kwanini umeweka hawa watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, nawe unaingia ndani kwa kushindwa kuwaweka ndani hawa watuhumiwa, RPC muweke ndani sasa hivi huyu,” alisema Lugola akiwa amekasirika. 

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo (RPC), Mkondya alimweleza Waziri Lugola kituoni hapo kuwa, Polisi wake walifanya makosa kwa kutowaweka mahabusu watuhumiwa hao.

Kwa upande wake mkuu wa kituo huyo, Mhando kabla ya kuwekwa mahabusu pamoja na wale watuhumiwa ambao alishindwa kuwaweka mahabusu, alisema sababu kuu yakutowaweka mahabusu watuhumiwa hao ni kwasababu mahabusu ilijaa na wanafanya hivyo mara chache inapotokea mahabusu wamekuwa wengi kituoni hapo. 


Hivyo makala LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA

yaani makala yote LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/lugola-amsweka-ndani-mkuu-wa-kituo_27.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA"

Post a Comment

Loading...