Loading...

MAJALIWA - VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA

Loading...
MAJALIWA - VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAJALIWA - VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAJALIWA - VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA
link : MAJALIWA - VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA

soma pia


MAJALIWA - VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA

Mwambawahabari
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wabadilike na watafakari namna bora ya kuboresha maisha yao na wafanye kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kulalamika.

Amesema kama kuna changamoto zinawakabili katika utekelezaji wa shughuli zao, basi watumie njia sahihi ikiwemo kuwasilina na viongozi husika waliopo kwenye maeneo yao.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumatano, Agosti 8, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye zahanati ya kijiji cha Nandagala.

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mary Majaliwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa, alisema vijana wanatakiwa kujitambua na kuiunga mkono Serikali kwa kufanyakazi kwa bidii.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka vijana washirikiane kwa pamoja katika kubuni shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato, jambo ambalo litawakwamua kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao mikakati mbalimbali inayofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya wilaya hiyo ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya pamoja na maji safi na salama.
PiaWaziri Mkuu aliwataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 9, 2018.


Hivyo makala MAJALIWA - VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA

yaani makala yote MAJALIWA - VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAJALIWA - VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/majaliwa-vijana-fanyeni-kazi-acheni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAJALIWA - VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA"

Post a Comment

Loading...