Loading...
title : MAOMBI YA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA SWAHILI FASHION WEEK WASHNGTON BENBELLA EMERGING DESIGNER YAMEANZA RASMI
link : MAOMBI YA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA SWAHILI FASHION WEEK WASHNGTON BENBELLA EMERGING DESIGNER YAMEANZA RASMI
MAOMBI YA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA SWAHILI FASHION WEEK WASHNGTON BENBELLA EMERGING DESIGNER YAMEANZA RASMI
Kwa kipindi cha miaka 10, maonyesho ya mavazi ya Swahili Fashion Week yamebaki kuwa mbele katika kutoa na kuwatengenezea njia wabunifu chipukizi katika tasnia ya mitindo Afrika mashariki na kati. Swahili fashion week kupitia shindano la kutafuta mbunifu chipukizi lijulikanalo kama Washington Benbella Emerging Designer Competition (WB-EDC) limekuwa likisherehekea vipaji vingi vya mitindo mbalimbali barani afrika na vile vile wabunifu chipukizi wamekuwa wakipata kujiamini na kuweza kuanzisha bidhaa zao.
Mwaka huu, katika mashindano haya yakiwa na dhima kuu ya “kukuza lugha ya Kiswahili” yamefungua rasmi milango kwa wabunifu vijana barani afrika kutuma maombi kwa fursa hii ya kipekee itakayo mpa nafasi ya kutambulika katika tasni ya mitindo na kupata uzoefu.
“tunafurahi fungua awamu ya 11 ya mashindano haya, na siku zote huwa tuna furaha ya kutoa fursa za thamani kwa wabunifu chipukizi wenye vipaji na hamasa ambao watawakilisha tasnia ya mitindo barani afrika kwa miaka ijayo. Hivyo tunawasihi wabunifu wote chipukizi kuikumbatia fursa hii kwa umakini na kutuma maombi kabla ya tarehe 30 Septemba 2018 saa 12 jioni.” Alisema Afisa uhusiano wa Swahili Fashion Week, Maryam Idriss.
Chipukizi 10 watakaochaguliwa kuingia fainali, watapewa nafasi ya kuonyesha mitindo ya nguo zao katika siku ya pili ya maonyesho ya Swahili Fashion Week ambayo itakuwa ni tarehe 1 Disemba 2018, kasha majaji watachagua mshindi na atazawadia tuzo na nafasi ya kushiriki na kuonyesha mavazi yake mengi zaidi katika maonyesho ya 12 ya Swahili Fashion Week mwaka 2019.
Fomu za maombi tayari zipo kwenye tovuti https://ift.tt/1R2Cuyj, tarehe ya mwisho wa kuwasilisha fomu ni 30 Septemba 2018 saa 12 za EAT. Waombaji wanakumbushwa kusoma maelekezo kwa makini ili wawasilishe maombi kamili.
Hivyo makala MAOMBI YA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA SWAHILI FASHION WEEK WASHNGTON BENBELLA EMERGING DESIGNER YAMEANZA RASMI
yaani makala yote MAOMBI YA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA SWAHILI FASHION WEEK WASHNGTON BENBELLA EMERGING DESIGNER YAMEANZA RASMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAOMBI YA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA SWAHILI FASHION WEEK WASHNGTON BENBELLA EMERGING DESIGNER YAMEANZA RASMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/maombi-ya-kushiriki-katika-mashindano.html
0 Response to "MAOMBI YA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA SWAHILI FASHION WEEK WASHNGTON BENBELLA EMERGING DESIGNER YAMEANZA RASMI"
Post a Comment