Loading...
title : MBUNGE JANETH MASABURI AHITIMISHA ZIARA,AZUNGUMZA NA WANA CCM JIMBO LA UKONGA ATOA USIA MZITO.
link : MBUNGE JANETH MASABURI AHITIMISHA ZIARA,AZUNGUMZA NA WANA CCM JIMBO LA UKONGA ATOA USIA MZITO.
MBUNGE JANETH MASABURI AHITIMISHA ZIARA,AZUNGUMZA NA WANA CCM JIMBO LA UKONGA ATOA USIA MZITO.
Na. John Luhende
Mwamba wa habari
Mbunge wa kuteuliwa Mama Janeth Masaburi amehitimisha ziara yake ya sikutatu yakutembela mkoa wa Dar es salaam kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi .
Mbunge Masaburi amehitimisha ziara hiyo kwa kuzungumza na wanachama na wenyeviti na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM Kitunda na Kivule ,ambapo amewataka viongozi na wanachama kushikamana kwa pamoja ilikuhakikisha Ukonga wanaikomboa kuoka upinzani katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na na jimbo lote la ukonga lina kuwa chini ya CCM.
“Lazima tubaini kero zote zilizopo katika mitaa yetu mapema na kuzitatua ili tusije kutumia jasho jingi Damu kidogo wakati wa vita tutatoa jasho kidogo na hatuta hema sana wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa” alisema .
“Lazima tubaini kero zote zilizopo katika mitaa yetu mapema na kuzitatua ili tusije kutumia jasho jingi Damu kidogo wakati wa vita tutatoa jasho kidogo na hatuta hema sana wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa” alisema .
Aidha amewataka kuacha ubinafsi na nongwa ilikupata viongozi wanafanyakazi kwaajili ya kuwaletea maendeleo wananchi na kuwataka kuelewa kuwa serika msingi wake ni serikali za mitaa ili kupata viongozi bora kunahitaji mshikamano.
“Upinzani tuliuruhusuwenyewe kwa sababu ya ubinafi mmeona wenyewe mlipata kunyapaliwa mkitaka huduma mlinyimwa hadi vyandarua mlinyimwa , kunasiku utataka huduma au ndugu yako atataka huduma atazikosa kwa kwasababu wewe ulitumia wivu tu kwa kumkomoa mtu kwa makosa madogomadogo acheni wivu.” Alisema.
Hatahivyo Masaburi, amewataka wajumbe hao kuwanyenyekea wanachama na wananchi kwakuwa wao wakopale kwaajili yakuwatumikia.
Katika ziara hiyo Janeth Masaburi ameatembelea maeneo yahuduma za kijamii ikiwemo kituo cha afya Buguruni mnyamani , pamoja na kupongeza huduma nzuri zinazotolewa ,ameutaka uongozi wa kituo hicho pamoja kuweka mikakati madhubuti ilikuboreshahuduma ikiwemo upanuzi wa eneo na kufikiria kujenga Majengo ya ghorofa, pia akawataka wakala wa baraba za mjini na Vijijini TARURA kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Buguruni kwa myamani ili kuondoa usumbufu wanao upata wanachi hasa wanao enda kutibiwa katika Kituo cha Afya Buguruni kwa Mnyamani .
Maeneo mengine aliyo tembelea ni pamokoja na mradi wa visima virefu vya maji Wilaya Kigamboni ambao unatekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, Dar es Salaam (DAWASA)
Mhe. Masaburi amesema kuwa ni vyema serikali ikaongeza nguvu katika kukamilisha mradi huo wa maji ambao utakuwa msaada katika kuondoa na kero ya ukosefu wa maji.
"Mradi huu ukikamilika wakazi wa Dar es Salaam itakuwa historia kuhusu ukosefu wa maji" amesema Mhe. Masaburi.
Amesema kuwa visima hivyo vina maji ya kutosha, hivyo wananchi wanapaswa kutunza vyanzo vya maji ili kuhakikisha vinawasaidia.
Mhe. Masaburi amesema kuwa serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ili kuhakikisha inatatua changamoto ambazo zimekuwa kikwazo katika maendeleo.
"Naipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitahada zake katika kuhakikisha inatekeleza miradi ya kimaendeleo" Ukitaka kuifahamu CCM nenda site" amesema Masaburi na kuongeza.
Hivyo makala MBUNGE JANETH MASABURI AHITIMISHA ZIARA,AZUNGUMZA NA WANA CCM JIMBO LA UKONGA ATOA USIA MZITO.
yaani makala yote MBUNGE JANETH MASABURI AHITIMISHA ZIARA,AZUNGUMZA NA WANA CCM JIMBO LA UKONGA ATOA USIA MZITO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE JANETH MASABURI AHITIMISHA ZIARA,AZUNGUMZA NA WANA CCM JIMBO LA UKONGA ATOA USIA MZITO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mbunge-janeth-masaburi-ahitimisha.html
0 Response to "MBUNGE JANETH MASABURI AHITIMISHA ZIARA,AZUNGUMZA NA WANA CCM JIMBO LA UKONGA ATOA USIA MZITO."
Post a Comment