Loading...
title : MBUNGE JANETH MASABURI: SERIKALI INATAKIWA KUONGEZA NGUVU MRADI WA MAJI KIMBIJI ILI TATIZO LA MAJI DAR IWE HISTORIA
link : MBUNGE JANETH MASABURI: SERIKALI INATAKIWA KUONGEZA NGUVU MRADI WA MAJI KIMBIJI ILI TATIZO LA MAJI DAR IWE HISTORIA
MBUNGE JANETH MASABURI: SERIKALI INATAKIWA KUONGEZA NGUVU MRADI WA MAJI KIMBIJI ILI TATIZO LA MAJI DAR IWE HISTORIA
Miongoni mwa visima 20 vilivyopo kimbiji Wilaya ya Kigamboni.
Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Janeth Masaburi akifanya ukaguzi katika kisima kirefu cha maji Kimbiji leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake kukagua miradi mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Janeth Masaburi imeitaka Serikali kupitia sekta husika kukamilisha mradi wa visima virefu vya maji Kimbiji jambo ambalo litasaidia kuondoa kero ukosefu wa maji katika Jiji la Dar es Salaam.
Mhe. Masaburi ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara ya kukagua mradi wa visima virefu vya maji Wilaya Kigamboni ambao unatekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, Dar es Salaam (DAWASA).
Mhe. Masaburi amesema kuwa ni vyema serikali ikaongeza nguvu katika kukamilisha mradi huo wa maji ambao utakuwa msaada katika kuondoa na kero ya ukosefu wa maji.
"Mradi huu ukikamilika wakazi wa Dar es Salaam itakuwa historia kuhusu ukosefu wa maji" amesema Mhe. Masaburi.
Amesema kuwa visima hivyo vina maji ya kutosha, hivyo wananchi wanapaswa kutunza vyanzo vya maji ili kuhakikisha vinawasaidia.
Mhe. Masaburi amesema kuwa serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ili kuhakikisha inatatua changamoto ambazo zimekuwa kikwazo katika maendeleo.
"Naipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitahada zake katika kuhakikisha inatekeleza miradi ya kimaendeleo" amesema Mhe. Masaburi.
Hata hivyo amefafanua kuwa miaka kadhaa iliyopita kuliwa na shida ya maji katika maeneo mengi ya jijini la Dar es Salaam, lakini kwa sasa asilimia kubwa ya maeneo hayo kuna huduma ya majii
Katika hatua nyengine Mhe. Masaburi ametembelea Ofisi ya CCM Kata ya Kigamboni na kuwapongea wanachama wa kata hiyo katika jitihada za kufanikisha shughuli za kimaendeleo pamoja na kumchagua Mhe. Faustine Ndugulile kuwa mbunge wa Jimbo la kigamboni.
Ameeleza kuwa Jimbo la Kigamboni linapaswa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mhe. Ndugulile ambaye amekuwa akisimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo.
"Ukitaka kujua utekelezaji Ilani ya CCM nenda site...utaona watu wanavyofanya kazi katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo" amesema Mhe. Masaburi.
Kwa upande wake Mhe. Ndugulile amesema kuwa serikali inaendelea kufanya kazi ili kutatua changamoto za wananchi.
Mhe. Ndungulile ambaye ni Naibu Waziri Afya, Ustawi wa jamii Wazee na Watoto, amesema kuwa mpaka sasa tayari kila hospitali kuna dawa za kutosha.
"Pamoja na juhudi za serikali mimi nitahakikisha huduma za Afya zinapatika na kama kuna mtu anafanya ujanja ujanja nitamchukia hatua" amesema Mhe. Ndugulile.
Hivyo makala MBUNGE JANETH MASABURI: SERIKALI INATAKIWA KUONGEZA NGUVU MRADI WA MAJI KIMBIJI ILI TATIZO LA MAJI DAR IWE HISTORIA
yaani makala yote MBUNGE JANETH MASABURI: SERIKALI INATAKIWA KUONGEZA NGUVU MRADI WA MAJI KIMBIJI ILI TATIZO LA MAJI DAR IWE HISTORIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE JANETH MASABURI: SERIKALI INATAKIWA KUONGEZA NGUVU MRADI WA MAJI KIMBIJI ILI TATIZO LA MAJI DAR IWE HISTORIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mbunge-janeth-masaburi-serikali.html
0 Response to "MBUNGE JANETH MASABURI: SERIKALI INATAKIWA KUONGEZA NGUVU MRADI WA MAJI KIMBIJI ILI TATIZO LA MAJI DAR IWE HISTORIA"
Post a Comment