Loading...

MIKUTANO YA JPC NI INJINI YA MAENDELEO YA KIUCHUMI, BALOZI MAHIGA

Loading...
MIKUTANO YA JPC NI INJINI YA MAENDELEO YA KIUCHUMI, BALOZI MAHIGA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MIKUTANO YA JPC NI INJINI YA MAENDELEO YA KIUCHUMI, BALOZI MAHIGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MIKUTANO YA JPC NI INJINI YA MAENDELEO YA KIUCHUMI, BALOZI MAHIGA
link : MIKUTANO YA JPC NI INJINI YA MAENDELEO YA KIUCHUMI, BALOZI MAHIGA

soma pia


MIKUTANO YA JPC NI INJINI YA MAENDELEO YA KIUCHUMI, BALOZI MAHIGA


Tanzania na Uganda zimepata mafanikio makubwa kupitia Mikutano ya Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) iliyofanyika Arusha Aprili 2017 na sasa wa Kampala unaohitimishwa leo.

Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhe .Dkt. Augustine Mahiga (Mb) na mwenzake wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa walipokuwa wanasoma hotuba za ufunguzi wa mkutano huo.

Mafanikio yaliyoelezwa ni pamoja na kusainiwa kwa Mikataba ya Makubaliano tisa ikiwemo Mikataba ya kushirikiana katika uendelezaji wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Dar Es Salaam hadi Uganda na ushirikiano katika masuala ya elimu na mafunzo iliyosainiwa leo katika mkutano wa Kampala.

Mkutano huo ulijulishwa kuwa utekelezaji wa mikataba hiyo unaridhisha na inalenga kurahisisha ukuaji wa uchumi wa nchi hizo ili kutimiza azma ya viongozi wake, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mhe. Yoweri Museveni wa Uganda ya kukuza biashara kati ya nchi hizo.Mikataba iliyosainiwa inahusu uendelezaji wa miradi ya miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na nishati ya Umeme, barabara hususan za mipakani, bandari, reli na usafiri wa anga. 

Kufuatia mikataba hiyo miradi mbalimbali ipo katika hatua tofauti za utekelezaji ikiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa Kikagati/ Murongo uliopangwa kukamilika mwaka 2020. Aidha, Shirika la Ndege la Tanzania litaanza safari za moja kwa moja kutoka Dar Es Salaam hadi Entebbe mwishoni mwa mwezi huu kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa masuala ya anga katika mkutano wa Arusha mwezi Aprili 2018
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) na Waziri wa Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhe. Peter T. Lokeris wakiweka saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kuendeleza ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Dar Es Salaam hadi Uganda. Aliyesimama kushoto kwa Mhe. Mahiga ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akibadilishana Mikataba na Waziri wa Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhe. Peter T. Lokeris baada ya kusainiwa. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Elimu ya Juu wa Uganda, Mhe. J.C Muyingo wakiweka saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kushirikiana katika masuala ya Elimu na Mafunzo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Elimu ya Juu wa Uganda, Mhe. J.C Muyingo wakibadilishna Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kushirikiana katika masuala ya Elimu na Mafunzo. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa akimkabidhi Hati za Viwanja va Ubalozi wa Tanania nchini Uganda Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, Balozi Patrick Mugoya (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi wakibadilishana taarifa ya masuala yote yaliyoafikiwa katika mkutano huo. 



Hivyo makala MIKUTANO YA JPC NI INJINI YA MAENDELEO YA KIUCHUMI, BALOZI MAHIGA

yaani makala yote MIKUTANO YA JPC NI INJINI YA MAENDELEO YA KIUCHUMI, BALOZI MAHIGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MIKUTANO YA JPC NI INJINI YA MAENDELEO YA KIUCHUMI, BALOZI MAHIGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mikutano-ya-jpc-ni-injini-ya-maendeleo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MIKUTANO YA JPC NI INJINI YA MAENDELEO YA KIUCHUMI, BALOZI MAHIGA"

Post a Comment

Loading...