Loading...

MKUU MPYA WA WILAYA KISARAWE JOKATE APISHWA

Loading...
MKUU MPYA WA WILAYA KISARAWE JOKATE APISHWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKUU MPYA WA WILAYA KISARAWE JOKATE APISHWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKUU MPYA WA WILAYA KISARAWE JOKATE APISHWA
link : MKUU MPYA WA WILAYA KISARAWE JOKATE APISHWA

soma pia


MKUU MPYA WA WILAYA KISARAWE JOKATE APISHWA

Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akiapishwa leo.

 Mwambawahabari.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo pamoja na Zainab Kawawa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo wameapisha leo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Jokate, ambaye aliwahi kuwa mlimbwende wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006, aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Julai 28 mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya wakuu hao wawili wa wilaya kuapishwa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani, Ramadhani Maneno amewataka wateule hao waepuke wanaofika ofisini kutaka kuwapotosha katika utendaji wao.

Amewataka wakakae na makatibu tawala ili wakusanye mapato kwani mkoa wa Pwani una viwanda.

“Kwa nafasi mlizopata hakikisheni mnakua karibu na viongozi wa chama hilo ni jambo kubwa. Wakati sasa mnaenda kuripoti kwenye wilaya mkaanzie kwenye ofisi za chama,”amesema.

Ameongeza: "Huko mnapoenda mtafute desturi na mila za maeneo yenu msizipuuzie, lakini mtafute yale yanayoendana na nyaraka zilizopo.”

Amesema anawakabidhi vitu vitatu, macho, masikio na mdomo ambavyo vitawasaidia kwenye utendaji wao wa kazi.

Pamoja na kuwepo kwa idadi ndogo ya waliohudhuria sherehe hizo za uapisho, hakuna msanii hata mmoja aliyeonekana.

Wengi walitarajia kuona wasanii wakijitokeza kwa wingi katika sherehe hizo kwa kuwa Jokate ni msanii wa filamu, muziki na ni mwanamitindo.


Hivyo makala MKUU MPYA WA WILAYA KISARAWE JOKATE APISHWA

yaani makala yote MKUU MPYA WA WILAYA KISARAWE JOKATE APISHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKUU MPYA WA WILAYA KISARAWE JOKATE APISHWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mkuu-mpya-wa-wilaya-kisarawe-jokate.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MKUU MPYA WA WILAYA KISARAWE JOKATE APISHWA"

Post a Comment

Loading...