Loading...
title : MKUU WA WILAYA NAMTUMBO AWAOMBA WAWEKEZAJI KUJENGA KIWANDA CHA SOYA ILI KUONGEZA THAMANI YA ZAO HILO
link : MKUU WA WILAYA NAMTUMBO AWAOMBA WAWEKEZAJI KUJENGA KIWANDA CHA SOYA ILI KUONGEZA THAMANI YA ZAO HILO
MKUU WA WILAYA NAMTUMBO AWAOMBA WAWEKEZAJI KUJENGA KIWANDA CHA SOYA ILI KUONGEZA THAMANI YA ZAO HILO
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume ametoa ombi kwa wawekezaji kuwekeza kwa kujenga kiwanda ambacho kitaisaidia kuongeza thamani ya zao la Soya ambalo linalimwa kwa wingi wilayani hapo.
Mfaume ametoa ombi hilo leo wakati anazungumzia jitihada zinazofanywa na wakulima wa Wilaya ya Namtumbo na hasa katika zao la Soya.
Amesema ombi kubwa ni kupata kiwanda cha Soya ndani ya Wilaya ya Namtumbo kwani kitakapojengwa kitasaidia kuongeza thamani ya zao la Soya."Tunaomba muwekezaji iwe anatoka Marekani au Taifa lolote aje awekeze kwa kujenga kiwanda cha kuchakata Soya kwa lengo la kuongeza thamani ya zao hili.
" Kwa mwaka huu wakulima wamepata tani 50,000 za Soya na kukiwa na kiwanda ambacho kitasaidia kuongeza thamani wanaweza kuzalisha zaidi ya tani za mwaka huu,"amesema.
Mfaume amesema kuwa mbali ya kuomba kiwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya zao la Soya ,pia ombi lao lingine ni kiwanda cha mbolea.Amefafanua changamoto waliyonayo wakulima ni mbolea na hivyo kukiwa na kiwanda katika wilaya hiyo watakuwa na uhakika wa mbolea na hivyo kuongeza uzalishaji.
Awali wakati anazungumzia zao la Soya amesema wakulima wengi wanalitumia zao hilo kwa chakula na chakuka cha wanyama.Amefafanua kuwa Soya inaweza kuzalisha maziwa,Soseji na nyama lakini hiyo ili ifanyike kunahitajika kiwanda cha kuchakata Soya.
Hivyo makala MKUU WA WILAYA NAMTUMBO AWAOMBA WAWEKEZAJI KUJENGA KIWANDA CHA SOYA ILI KUONGEZA THAMANI YA ZAO HILO
yaani makala yote MKUU WA WILAYA NAMTUMBO AWAOMBA WAWEKEZAJI KUJENGA KIWANDA CHA SOYA ILI KUONGEZA THAMANI YA ZAO HILO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA WILAYA NAMTUMBO AWAOMBA WAWEKEZAJI KUJENGA KIWANDA CHA SOYA ILI KUONGEZA THAMANI YA ZAO HILO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mkuu-wa-wilaya-namtumbo-awaomba.html
0 Response to "MKUU WA WILAYA NAMTUMBO AWAOMBA WAWEKEZAJI KUJENGA KIWANDA CHA SOYA ILI KUONGEZA THAMANI YA ZAO HILO"
Post a Comment