Loading...

MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI.

Loading...
MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI.
link : MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI.

soma pia


MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI.


Mtawa Suzan Bathlomeo enzi za uhai wake
Mkurugenzi wa Fedha na Mipango katika Hospitali ya Rufaa Bugando, jijini Mwanza, Mtawa Suzan Bathlomeo amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani muda mfupi baada ya kutoka kusali misa ya saa 12:00 asubuhi leo Jumanne Agosti 28, 2018.

Inaelezwa kuwa mtawa huyo amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo na kusababisha kuumia maeneo ya kiuno na mgongo.

Afisa Uhusiano wa Bugando Lucy Mogele amesema hospitali hiyo haina mamlaka ya kuzungumzia suala hilo na kutaka litafutwe shirika la watawa la Kagera ambalo makao makuu yake yapo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

“Ni kweli Sister Suzan amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani lakini Bugando hatuna mamlaka ya kuzungumzia suala hilo” ,alisema Lucy.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa Polisi Jonathan Shana amethibitisha kutokea kwa tukio na kwamba chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa.

"Bado tupo katika upelelezi kuhusiana na tukio hili,mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi na pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi", alisema.

Aidha ametoa wito kwa wananchi mkoani Mwanza kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi wanapoona wamekwenda kinyume na taratibu za kazi kama vile kujitoa uhai au kujijeruhi kwani ni kosa kisheria.

Habari kutoka hospitalini hapo zinabainisha kuwa katika ofisi aliyokuwa akiifanyia kazi mtawa huyo ambapo yeye alikuwa kiongozi kuna tuhuma za upotevu wa fedha zaidi ya milioni 300 ambazo zilipelekea baadhi ya watumishi wenzake kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi na wengine kufukuzwa kazi


Hivyo makala MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI.

yaani makala yote MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mtawa-ajiua-kwa-kujirusha-ghorofani.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI."

Post a Comment

Loading...