Loading...
title : Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni kuwasili kesho kwa ziara ya siku moja nchini
link : Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni kuwasili kesho kwa ziara ya siku moja nchini
Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni kuwasili kesho kwa ziara ya siku moja nchini
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni atafanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini tarehe 09 Agosti 2018.
Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema uliopo kati ya Tanzania na Uganda.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Rais Museveni atapokelewa na mwenyeji wake Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiwa nchini, Mheshimiwa Rais Museveni atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Mheshimiwa Rais Magufuli yatakayofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yatafuatiwa na Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Mheshimiwa Rais Magufuli kwa heshima ya Mheshimiwa Rais Museveni.
Mheshimiwa Rais Museveni na Ujumbe wake wataondoka nchini siku hiyo hiyo kurejea Uganda.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
07 Agosti 2018
Hivyo makala Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni kuwasili kesho kwa ziara ya siku moja nchini
yaani makala yote Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni kuwasili kesho kwa ziara ya siku moja nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni kuwasili kesho kwa ziara ya siku moja nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/rais-wa-jamhuri-ya-uganda-yoweri-kaguta.html
0 Response to "Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni kuwasili kesho kwa ziara ya siku moja nchini"
Post a Comment