Loading...

RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini

Loading...
RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini
link : RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini

soma pia


RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini

 MKUU wa mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi ameahidi kushirikiana kikamilifu na wakuu wenzake wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutangaza fursa na vivutio vya kiutalii vinavyopatikana katika ukanda huo, ikiwa ni mwendelezo wa harakati za kuunga mkono adhma ya Rais John Pombe Magufuli ya kufungua na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.

Katika kuthibitisha hilo kwa vitendo, Bw Hapi ameahidi kuunga mkono jitihada zilizoanzishwa na mtangulizi wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Bi. Amina Masenza za kuyaboresha zaidi Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 yanayoenda sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani ambayo Kitaifa yatafanyika mkoani Iringa Septemba 26 hadi 30 mwaka huu.

Bw Hapi ametaja mkakati wake huo, mapema wiki hii jijini Dar es Salaam alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Capital Plus International (CPI) inayoshirikiana na ofisi ya Mkuu wa Iringa pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kuratibu maonesho hayo yanayofanyika mjini Iringa kwa mwaka wa tatu mfululizo.

“Tungependa watu kutoka maeneo mengine ya Tanzania na hata nje ya nchi waje katika maonesho hayo ili waone na kutembelea vivutio vya utalii, kihistoria na kufahamu fursa za uwekezaji tulizo nazo”, alisisitiza kiongozi huyo wa Iringa.

‘’Mikoa ya nyanda za juu Kusini inasifika kuwa na hifadhi zenye sifa za kipekee ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye makundi makubwa ya tembo na wanyama wengine. Aidha, hifadhi ya Kitulo yenye aina mbali mbali za maua ambayo hayapatikani mahali pengine Duniani na Udzungwa yenye wanyama na viumbe adimu duniani kama vyura wa Kihansi,’’ alitaja

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi (katikati) akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Capital Plus Internantional kuhusiana na maandalizi ya Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 alipotembelea ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kampuni ya Capital Plus International inashirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuandaa maonesho hayo yanayotarajiwa kufanyika Septemba 26 hadi 30 mwaka huu kwenye Viwanja vya Kihesa Kilolo mkoani Iringa yakihusisha mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini. 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi (kulia)akipokea zawadi ya kikombe maalumu chenye nembo ya Capital Plus Internantional kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni hiyo Bi Farida Adam ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kwenye ofisi hizo. Capital Plus Internantional inashirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Iringa kuandaa maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018. 

Mratibu wa Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 kutoka kampuni ya Capital Plus Internantional Bw Clement Mshana akifafanua jambo kwa Mkuu  wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi kuhusu maandalizi ya Maonesho hayo wakati wa kikao hicho.
Mratibu Msaidizi wa Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 kutoka kampuni ya Capital Plus Internantional Bw Malela Kassim (katikati) akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya Maonesho hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi (hayupo pichani)wakati wa kikao hicho.



Hivyo makala RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini

yaani makala yote RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/rc-hapi-aahidi-kuboresha-sekta-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini"

Post a Comment

Loading...