Loading...

Redcross Tanzania imedhamiria katika utoaji wa elimu ya huduma ya Kwanza.

Loading...
Redcross Tanzania imedhamiria katika utoaji wa elimu ya huduma ya Kwanza. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Redcross Tanzania imedhamiria katika utoaji wa elimu ya huduma ya Kwanza., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Redcross Tanzania imedhamiria katika utoaji wa elimu ya huduma ya Kwanza.
link : Redcross Tanzania imedhamiria katika utoaji wa elimu ya huduma ya Kwanza.

soma pia


Redcross Tanzania imedhamiria katika utoaji wa elimu ya huduma ya Kwanza.

 Katibu Mkuu wa Recross Tanzania Julius Kejo akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na kazi ya Redcross katika utoaji wa huduma wakati wa Majanga yanapotokea, mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Ubelgiji Red cross Tanzania An Vanderheyden akizungumza uzoefu wa Redcross katika kujitoa katika uchangiaji.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
REDCROSS Tanzania imedhamiria kuleta mapinduzi kwa wananchi kuhakikisha kila mmoja anawajibika kutoa msaada wa majanga yanayojitokeza ili kusaidia waathirika wa majanga hayo wasipoteze maisha kwa kukosa huduma ya kwanza.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Redcross Julius Kejo wakati akizungumza na waandishi habari kuhusiana kazi zinazofanywa na Redcross Tanzania na namna kuhakikisha jamii inawajibika kusaidia kuwa mstari wa mbele katika majanga mbalimbali yanayotokea na kuachana na tabia ya kukimbilia kuona bila ya msaada wa huduma ya kwanza.

Amesema bado kuna tatizo kubwa kwa jamii kutowajibika pale yanapotokea majanga ikiwamo ya ajali na mengineyo kwa kushindwa kuwasaidia kwa haraka watu wanaopata athari katika majanga hayo badala yake kubaki washudiaji tu na kupiga picha.

“Ajali ikitokea, badala ya watu kutoa msaada wa huduma ya kwanza kuokoa maisha yao, watu wanawazunguka kuwashangaa, na wengine wanatumia muda huo kuchukua picha kutuma kwenye mitandao na kuacha wenzao wakihangaika au baadhi ya wengine wanapoteza maisha wakati huo huo kwa kukosa huduma ya kwanza wakati pengine wangewasaidi kuokoa maisha yao ,” amesema Kejo

Amesema umefika wakati watanzania kubadilika kujitoa katika kupata elimu ya huduma ya kwanza ambayo itatumika katika kuokoa maisha ya watu katika majanaga mabalimbali kwani kusaidia mtu katika majanga ni haki kwa yule yaliyompata.

"Tuwe na huruma kila mmoja awajibike tusikubali kuwapoteza ndugu nzetu na nguvu kazi ya taifa letu kwa vitu ambavyo hata sisi tunaweza kutoa msaada bila kutegemea msaada kutoka kwa watu wengine kutoka nje.”

Amesema kwa sasa Redcross watahakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa kila mmoja kuanzia ngazi ya familia, mikoa yote, mijini na vijijini kuhakikikisha kila mmoja anawajibika kutoa msaada wa huduma ya kwanza katika majanga ili kupunguza idadi ya watu wanaopata matatizo ama kufariki kutokana na kukosa msaada huo wa kwanza.

kwa upande wake, Kheri Ngwere, Mratibu wa Huduma ya Kwanza, Redcross, amesema wako kwenye mchakato wa kuandaa mtaala wa namna ya utoaji wa huduma ya kwanza ambao unatarajiwa kutumika katika taasisi mbalimbali hasa zinazotoa mafunzo ya ufundi stadi na usalama balabalani.

Amesema wanatarajia mtaala huo utaanza kutumika Septemba mwaka huu kwa majaribio kwa kipindi cha miezi sita na baadae kuanza kutumika rasmi na kwamba lengo ni kuwajenhea uwezo jamii kuokoa maisha ya watu kwenye majanga kupitia huduma hiyo ya kwanza.


Hivyo makala Redcross Tanzania imedhamiria katika utoaji wa elimu ya huduma ya Kwanza.

yaani makala yote Redcross Tanzania imedhamiria katika utoaji wa elimu ya huduma ya Kwanza. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Redcross Tanzania imedhamiria katika utoaji wa elimu ya huduma ya Kwanza. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/redcross-tanzania-imedhamiria-katika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Redcross Tanzania imedhamiria katika utoaji wa elimu ya huduma ya Kwanza."

Post a Comment

Loading...