Loading...

Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma

Loading...
Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma
link : Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma

soma pia


Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma


Wanafunzi wa darasa la Saba Shule ya Uhuru Wasichana ambao wamemaliza Shule wakiwaaga wenzao ambao wanabaki katika mahafali ya 58 ya Shule hiyo Dar es salaam Leo (Picha na Heri Shaban)

Na Heri Shaban
Mwambawahabari
SHULE ya Msingi Uhuru Wasichana Iliyopo Wilayani Ilala wajivunia mafanikio kwa upande wa taaluma imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa kila mwaka.


Ofisa Tarafa KARIAKOO Christina Kelekezi akizunngumza katika mahafali ya 58 ya darasa la Saba Saba Shule ya Uhuru Wasichana Dar es salaam Leo (kulia) Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Christina Wambura (Picha na Heri Shaban)

Hayo yalisemwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Christina Wambura wakati wa mahafali ya 58 ya darasa la saba ya shule hiyo.

Wambura alisema shule ya UHURU Wasichana ilianza mwaka 1932 katika Mtaa wa Bagamoyo ikiwa na wanafunzi nane mwaka 1934 iliongezeka ikafikia wanafunzi 60 ilipo fika mwaka 1935 Shule hiyo iliamishiwa mtaa wa Kichwele na kuitwa Kichwele Girls  Mara baada kupata UHURU Shule ikapewa jina Uhuru Wasichana Shule pekee ya Wasichana hapa nchini.

"Shule yetu katika taaluma ipo vizuri mwaka 2015 darasa la nne na darasa la Saba walifaulu kwa asilimia 100 na mwaka 2016 darasa la nne walifaulu kwa asilimia 100 darasa la Saba walifaulu kwa asilimia 98 na mwaka 2017 darasa la nne na darasa la saba wote walifaulu kwa asilimia 100 "alisema Wambura.

Wambura alisema  kwa mwaka huu matarajio kufaulisha kwa asilimia 100 kutokana na kuandaliwa vizuri na Walimu na Wanafunzi wote wameonyesha bidii.


Akizungumzia mazingira ya Shule hiyo ni mazuri kwa  kufundishia na kujifunzia ambapo Shule imeshinda mashindano mbalimbali ya mazingira na kujinyakulia vikombe ngazi ya Mkoa na Wilaya kushika nafasi ya kwanza na pili.

Pia Shule ya Uhuru  Wasichana ina  mahabara ya Kisasa wanafunzi wanajifunza kwa vitendo  na walimu wao wanawafundisha kwa weledi.

Akizungumzia mahafali hayo ya 58 lengo na madhumuni kufanya sherehe hiyo kuwapongeza na kutoa motisha kwa wanafunzi wa darasa la Saba wanaohitimu ELIMU ya msingi mwaka 2018 kwa kutoa zawadi hasa wale waliofanya vizuri katika fani mbalimbali zikiwemo taaluma, nidhamu, usafi na michezo pia kujenga mahusiano mazuri baina ya uongozi wa Shule,walimu ,Wazazi na Wanafunzi.

Kwa upande wake mgeni rasmi Ofisa Tarafa KARIAKOO, Christina Kelekezi ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema alisema Watoto wa kike wanaweza wenyewe kwa kujiamini hivyo wamefungua njia ya mwanga bora  katika masomo wajiandae katika elimu ya SEKONDARI elimu aina mwisho.

Christina alisema kumaliza elimu ya msingi sio mwisho wa elimu bado wana kazi kubwa mbele ya kuendeleza elimu yao  hivyo aliwataka Wazazi kuwalea kwa maadili mema kama walivyofundishwa katika Shule hiyo.


Alipongeza mahabara ya Shule ya Uhuru Wasichana ipo vizuri na ni Shule ya kuaminika ya Serikali hapa nchini kushinda Shule zote.

Naye Diwani wa Kata ya GEREZANI FATUMA Abubar alisema elimu aina mwisho amewataka wanafunzi wazingatie masomo yao pindi wakiwa darasani na huko waendako wafuate maadili waliofundishwa katika Shule hiyo.




Hivyo makala Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma

yaani makala yote Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/shule-ya-msingi-uhuru-wasichana.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma"

Post a Comment

Loading...