Loading...
title : SIMBA KUSHUKA DIMBANI LEO ARUSHA
link : SIMBA KUSHUKA DIMBANI LEO ARUSHA
SIMBA KUSHUKA DIMBANI LEO ARUSHA
Na Noel Rukanuga, Dar es SalaamMabigwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba Sport Club leo wanatarajia kushika simbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Arusha United kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Simba inacheza mechi hiyo kwa mualiko maalumu wa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Mchezo huo utakuwa wa mwisho kwa ajili ya kujipima kabla ya kucheza na Mtibwa Sugar mechi ya ngao ya jamii utakaopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza mwishoni mwa wiki hii.
Mechi ya ngao ya jamii huashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu. Msimu wa 2018/19 unatarajiwa kuanza Agosti 22 mwaka huu.
Simba tangu irejee kutoka Uturuki ambako iliweka kambi ya wiki mbili, imeshacheza mechi mbili za kirafiki, dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana waliyotoka sare ya bao 1-1 na dhidi ya Namungo FC ya Lindi inayoshiriki Ligi daraja la kwanza ambapo walitoka suluhu.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Patric Aussems akizungumzia mechi hiyo alisema anaichukuliwa kwa uzito mechi hiyo kwani ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya ngao ya jamii.
“Tutautumia mchezo huo kama maandalizi ya mchezo wa ngao ya jamii, lakini kama nilivyosema hapo awali sisi ni washindani na tunahitaji kushinda zaidi kwa hiyo tunataka kuutumia vyema mchezo huo,”amesema Aussems.
Hivyo makala SIMBA KUSHUKA DIMBANI LEO ARUSHA
yaani makala yote SIMBA KUSHUKA DIMBANI LEO ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIMBA KUSHUKA DIMBANI LEO ARUSHA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/simba-kushuka-dimbani-leo-arusha.html
0 Response to "SIMBA KUSHUKA DIMBANI LEO ARUSHA"
Post a Comment