Loading...
title : TUNDU LISSU KUREJEA NCHINI KUWATUMIKIA WANANCHI.
link : TUNDU LISSU KUREJEA NCHINI KUWATUMIKIA WANANCHI.
TUNDU LISSU KUREJEA NCHINI KUWATUMIKIA WANANCHI.
Takriban miezi minane sasa tangu mwanasiasa wa upinzani na Mbunge wa Singida Mashariki nchini Tanzania Tundu Lissu kuwepo nchini Ubelgiji kwa ajili ya kupata matibabu.Kwa sasa mwanasiasa huyo anasema anataka kurudi nyumbani na kurejea katika shughuli zake za kisiasa kwa kuwa yeye bado ni mbunge na anahitajika kuwahudumia wananchi waliomchagua kwa kipindi cha miaka mitano.
Katika mazungumzo yake na mwandishi wa BBC, Zuhura Yunus ambaye alimtembelea hosptalini ,Tundu Lissu alibainisha hali ya upinzani nchini Tanzania kuwa ina mabadiliko makubwa tofauti na miaka ya nyuma.
Mwanasiasa huyo alidai kwamba wakati wa utawala wa rais Jakaya Kikwete , yeye alikuwa mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani kwa kipindi cha miaka mitano lakini hakuwahi kutishiwa.
katika kipindi chote cha miaka kumi ya uongozi wa Kikwete upinzani ulikuwa na makelele kweli kweli lakini haukuwahi kukutana na vitisho vya hali wanayoiona sasa.
Hali ilikuwa vivyo hivyo hata wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa licha ya kwamba alikuwa hajawa mbunge bado.
Lissu ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana katikati mwa ya mwaka jana na kufanyiwa upasuaji mara kadhaa hana uhakika atarejerea lini nchini Tanzania mpaka pale ambapo daktari atakapotoa ruhusa.
"Lazima nitarejea na nitakuwa na tahadhari zaidi maana ni jambo la lazima mimi kurudi,nikirejea nitaendelea kuwa kwenye siasa na wala siogopi kwa sababu bado mimi ni mbunge wa singida mashariki niliyechaguliwa na wananchi kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano"Lissu alisisitiza. Chanzo: Bbcswahili.
Hivyo makala TUNDU LISSU KUREJEA NCHINI KUWATUMIKIA WANANCHI.
yaani makala yote TUNDU LISSU KUREJEA NCHINI KUWATUMIKIA WANANCHI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUNDU LISSU KUREJEA NCHINI KUWATUMIKIA WANANCHI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/tundu-lissu-kurejea-nchini-kuwatumikia.html
0 Response to "TUNDU LISSU KUREJEA NCHINI KUWATUMIKIA WANANCHI."
Post a Comment