Loading...
title : ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA
link : ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA
ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA
Na Leandra Gabriel, Glogu ya jamii
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amechagia kiasi cha shilingi milioni 4.7 katika kata ya Nyamato, mifuko 250 ya Saruji kwaajili ya ujenzi wa vituo vya afya, shule na nyumba za Wauguzi hii ni katika kuhakikisha huduma za elimu na afya zinaimarika na kuwa faafu kwa wananchi wote wa Mkuranga.
Wakati huo huo Ulega pia ametoa amechangia shilingi laki sita kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Kimanzichana na ameahidi kutoa kiasi cha milioni 2 kwaajili ya vikundi vya wanawake wajasiriamali.
Akizungumza wakati wa utoaji wa mchango huo Ulega ameeleza kuwa ushirikiano wa wananchi unampa nguvu ya kufanya makubwa zaidi katika kuleta maendeleo na amewataka watendaji kufuata kasi iliyopo na kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa juhudi anazoonesha katika kuleta maendeleo nchini.
Pia Ulega amesema kuwa yupo pamoja na wananchi wa Mkuranga wakati wote na katika kufanya kila jambo litakaloleta maendeleo bila kujali itikadi wala chama.Katibu wa CCM Wilaya ya Mkuranga, Abihudi Shila ameeleza kuwa wanachama waendelee kufanya kazi na viongozi waliopo na amempongeza Rais kwa juhudi anazozifanya katika kuleta maendeleo hasa katika kukemea rushwa na ufisadi pia katika ujenzi wa miradi ya kimaendeleo nchini kama miradi ya umeme na miundombinu.
Aidha amemshukuru Rais kwa kumteua Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah Ulega katika kumsaidia kuongoza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kama naibu Waziri na wanashukuru kuona mbunge wao anafanya kazi kwa dhati katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Aidha Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamato Idd Kimbapule amempongeza Mbunge wa Mkuranga Abdalah Ulega kwa kutoa kipaumbele katika huduma muhimu kama afya, elimu na miundombinu na ameendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha shughuli za ujasiriamali kwa akina mama zinakuwa ili waweze kujipatia kipato.
Kimbapule amewashauri wananchi kuonesha ushirikiano kwa viongozi wa mfano wa Ulega ambaye amejitoa katika kuwahudumia wananchi ili kuweza kujenga maendeleo kwa kasi zaidi. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega akizungumza na wanachama wa CCM mara baada ya kukabidhi mifuko 250 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya shule pamoja na nyumba za waganga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega (kulia) akikabidhi Shilingi laki sita kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Kimanzichana ambapo pia aliahidi kuongeza milioni mbili kwa ajili ya vikundi vya wajasiliamali.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega akiwakabidhi kadi za (CCM) wanachama waliorudi wakitokea chama cha CUF Abed Majala, Modesta Antoni katika kijiji cha Kimanzichana Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Hivyo makala ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA
yaani makala yote ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/ulega-azidi-kuwakuna-wapiga-kura.html
0 Response to "ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA"
Post a Comment