Loading...
title : USHAURI WA JULIUS MTATIRO IWAPO ATAONANA NA RAIS DK. MAGUFULI HUU HAPA
link : USHAURI WA JULIUS MTATIRO IWAPO ATAONANA NA RAIS DK. MAGUFULI HUU HAPA
USHAURI WA JULIUS MTATIRO IWAPO ATAONANA NA RAIS DK. MAGUFULI HUU HAPA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KADA mpya wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Julius Mtatiro amesema iwapo atapata nafasi ya kuonana na Mwenyekiti wa Chama hicho kuna jambo la msingi ambalo anataka kumshauri kwa maslahi ya Watanzania walio wengi.
Mtatiro ambaye kabla ya kujiunga na CCM alikuwa Chama cha Wananchi(CUF) ambapo akiwa huko alishika nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za juu na sasa anasema baada ya kujiunga CCM anaoana ni kama ameutua mzigo mzito uliokuwa kichwani.
Akizungumza na Michuzi Blog katika mahojiano maalum yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Mtatiro amezungumzia mambo mbalimbali na kubwa ni kwamba viongozi wa ngazi zote za juu ndani ya CCM wamempokea na kumpa baraka na siku yoyote atachukua kadi.
Alipoulizwa iwapo atapata nafasi ya kuonana na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.John Magufuli Mtatiro amejibu iwapo atakutana naye atamshauri umuhimu wa kuongeza juhudi katika kupambana na umaskini nchini.Amesema anapongeza juhudi zinazoendelea katika kuondoa umaskini lakini ukweli ni kwamba umaskini bado mkubwa na anaamini Rais akifanikiwa katika hilo atakuwa ameondoa changamoto inayowakabili Watanzania wengi.
Amesema sababu za yeye kuamua kuingia katika siasa ni kutokana na hali ya umasikini uliopo kwenye familia anayotoka na jamii inayomzunguka.Hivyo anasema aliamini akiwa katika siasa atashiriki kuhamasisha na kuweka mipango ya maendeleo na ndio maana siku zote amekuwa akishauri namna bora ya kuondoa umaskini nchini.
"Jambo kubwa ambalo nitamueleza Mwenyekiti wangu wa CCM ni kumshauri aongeze kasi katika kuondoa hali ya umaskini kwani watanzania wengi wamezungukwa na umaskini." Ndio maana pamoja na sababu nyingi ambazo nimetoa wakati naondoka CUF moja ilikuwa ni kujiunga na CCM ili kama kijana na Mtanzania mzalendo nishiriki katika kuzungumzia na kuhamasisha maendeleo badala ya kukaa upande wa kupinga kila kinachofanyika,"amesema Mtatiro.
Alipoulizwa anajisikiaje anavyoshambuliwa na kutukanwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii,Mtatiro amejibu anaona na kusikia namna anavyotukanwa lakini haimuumizi kwani anaamini amefanya uamuzi sahihi.Amefafanua kabla kuondoka CUF amefanya utafiti wa kutosha kwa kuangalia aina ya siasa za upinzani, siasa za nchi na CCM na kuona sehemu sahihi ni huko alikokwenda sasa kwani yupo salama.

Hivyo makala USHAURI WA JULIUS MTATIRO IWAPO ATAONANA NA RAIS DK. MAGUFULI HUU HAPA
yaani makala yote USHAURI WA JULIUS MTATIRO IWAPO ATAONANA NA RAIS DK. MAGUFULI HUU HAPA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala USHAURI WA JULIUS MTATIRO IWAPO ATAONANA NA RAIS DK. MAGUFULI HUU HAPA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/ushauri-wa-julius-mtatiro-iwapo.html
0 Response to "USHAURI WA JULIUS MTATIRO IWAPO ATAONANA NA RAIS DK. MAGUFULI HUU HAPA"
Post a Comment