Loading...
title : VIBALI VYA UJENZI KUTOLEWA KILA WIKI.
link : VIBALI VYA UJENZI KUTOLEWA KILA WIKI.
VIBALI VYA UJENZI KUTOLEWA KILA WIKI.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kwamba kuanzia sasa vibali vya ujenzi vitakuwa vinatolewa kila wiki na vitakuwa vinatolewa na maafisa wa serikali waliopo wilayani ambao ni maafisa mipango miji, maafisa ardhi, wapimaji na wathamini ambao ni wataalamu.
“Kulikuwa na ucheleweshaji wa utoaji vibali vya ujenzi Mheshimiwa Rais ameshatoa maelekezo kwamba vibali vya ujenzi havitatolewa tena na kamati za madiwani kwasababu ilikuwa inachukua muda na walikuwa lazima walipwe posho, kwahiyo vibali vya ujenzi vitakuwa vinatoka kila wiki na vitatolewa na wataalamu wa serikali waliopo wilayani” amsema Mheshimiwa Lukuvi.
Amesema kwamba Serikali imeamua kubadili utaratibu huo ili kuwawezesha wananchi ambao walikuwa wana fedha ya kujenga maeneo yao lakini vibali vya ujenzi vilikuwa havitolewi kwa wakati, na kuna watu ambao walikuwa wanakaa mwaka mzima wakisubiri vibali vya ujenzi kitendo amabacho kilichangia ujenzi holela katika miji.
Mheshimiwa Lukuvi amesema serikali imeamua kuchukua hatua hizo ili kuondoa kero kwa wananchi ambao walikuwa wanapata tabu ya urasimu uliokuwepo hapo awali, kitu ambacho kilikuwa ni kikwazo katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesikiliza kero za migogoro ya ardhi ya wananchi zaidi ya 200 wa jiji la Arusha ambao walihudhuria katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Azimio la Arusha jijini hapo.
Hivyo makala VIBALI VYA UJENZI KUTOLEWA KILA WIKI.
yaani makala yote VIBALI VYA UJENZI KUTOLEWA KILA WIKI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIBALI VYA UJENZI KUTOLEWA KILA WIKI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/vibali-vya-ujenzi-kutolewa-kila-wiki.html
0 Response to "VIBALI VYA UJENZI KUTOLEWA KILA WIKI."
Post a Comment