Loading...

VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA

Loading...
VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA
link : VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA

soma pia


VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wabadilike na watafakari namna bora ya kuboresha maisha yao na wafanye kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kulalamika.

Amesema kama kuna changamoto zinawakabili katika utekelezaji wa shughuli zao, basi watumie njia sahihi ikiwemo kuwasilina na viongozi husika waliopo kwenye maeneo yao.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumatano, Agosti 8, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye zahanati ya kijiji cha Nandagala.Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mary Majaliwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa, alisema vijana wanatakiwa kujitambua na kuiunga mkono Serikali kwa kufanyakazi kwa bidii.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka vijana washirikiane kwa pamoja katika kubuni shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato, jambo ambalo litawakwamua kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao mikakati mbalimbali inayofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya wilaya hiyo ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya pamoja na maji safi na salama.

PiaWaziri Mkuu aliwataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani humo, Agosti 8.2018 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimshuhudia aliyekua Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mwita Waitara, akinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi, katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018
Aliyekua Mwenyekiti wa Kata ya Nandagala Jafari Omari (katikati), akikabidhi kadi yake ya CHADEMA kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, Agosti 8.2018 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Nandagala Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa kata ya Nandagala wakati akiwasili katika uwanja wa zahanati ya kijiji cha Nandagala kwa jailli ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, Agosti 8.2018.Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu


Hivyo makala VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA

yaani makala yote VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/vijana-fanyeni-kazi-acheni-kulalamika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA"

Post a Comment

Loading...