Loading...
title : Wafanyakazi 54 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Watunukiwa vyeti vya ufanyakazi bora
link : Wafanyakazi 54 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Watunukiwa vyeti vya ufanyakazi bora
Wafanyakazi 54 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Watunukiwa vyeti vya ufanyakazi bora
Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamesisitizwa kufanya kazi kwa bidii , na kuzingatia nidhamu katika utendaji wao ili kutoa huduma bora na yenye viwango vya juu.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru alipokuwa akizungumza katika hafla fupi ya kuwatunuku Vyeti wafanyakazi bora 54 wa Hospitali hiyo kwa mwaka 2018.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwatunuku vyeti wafanyakazi hao, amesema serikali inathamini mchango wa kila mmoja katika kuhudumia Umma hivyo wafanyakzi wote hawana budi kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa bidii bila kusukumwa.
‘’Nawapongeza kwakutoa huduma bora katika hospitali yetu naomba muendelee kuwa mabalozi wazuri , kwani mmekuwa mfano mzuri katika utekelezaji wa majukumu yenu ikiwa ni pamoja na utunzaji wa vifaa na kutoa lugha nzuri wakati wa kuwahudumiwa wateja’’. Amesema Prof. Museru.
Awali akikaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala Bwn. Makwaia Makani amesema wafanyakazi bora 54 hao wamewakilisha Idara mbalimbali, majengo na vitengo vya hospitali hiyo.
Prof: Museru akimkabidhi cheti cha ufanyakazi bora Theophil Joseph
Mmoja wa wafanyakazi bora Muuguzi Msaidizi Bi. Mkatareto Akyoo akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Prof. Museru.
Mfanyakazi bora kwa mwaka 2018 Philip Simya akikabidhiwa cheti mapema leo .
Wafanyakazi bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Prof; Lawrence Museru.
Hivyo makala Wafanyakazi 54 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Watunukiwa vyeti vya ufanyakazi bora
yaani makala yote Wafanyakazi 54 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Watunukiwa vyeti vya ufanyakazi bora Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wafanyakazi 54 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Watunukiwa vyeti vya ufanyakazi bora mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/wafanyakazi-54-wa-hospitali-ya-taifa.html
0 Response to "Wafanyakazi 54 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Watunukiwa vyeti vya ufanyakazi bora"
Post a Comment