Loading...
title : WATAALAM KUCHUNGUNZA UCHIMBAJI MADINI HIFADHI YA AMANI, TANGA
link : WATAALAM KUCHUNGUNZA UCHIMBAJI MADINI HIFADHI YA AMANI, TANGA
WATAALAM KUCHUNGUNZA UCHIMBAJI MADINI HIFADHI YA AMANI, TANGA
Na Zuena Msuya, Mheza ,Tanga
Serikali imesema itawaleta wataalam kutoka kituo cha Utafiti wa Miamba(GST), Wizara ya Maliasili na Mazingira kwenye eneo walilokuwa wakitumia wachimbaji wadogo kwa shughuli za madini, ambalo pia linadaiwa kuwa liko katika chanzo cha maji, kufanya utafiti na kujiridhisha kama eneo hilo liruhusiwe kuendeleza na shughuli za uchimbaji madini ama laa.
Hayo yalisemwa na Naibu waziri wa Madini Dotto Biteko alipotembelea katika kijiji cha Sakale katika Kata ya Mbomole Tarafa ya Amani wilayani Mheza mkoani Tanga, wakati akizungumza na wananchi waliomuelezea kero yao ya kuzuiwa na serikali kutokuchimba madini eneo hilo licha ya kuwatokuwepo na viashiria vya uharibifu wa mazingira na misitu kama serikali inavyosema.
Naibu Waziri Biteko, alisema kuwa kiu ya serikali ni kuwapatia maeneo ya uchimbaji wachimbaji wadogowadogo ili waweze kubadilisha maisha yao kupitia uchumi wa madini, hii ni kutokana Rais kubadilisha sheria za nchi kwa upande wa madini kutoka kuwanufaisha wageni na sasa kuwanufaisha watanzania.
“Serikali yenu ni sikivu,Mheshimiwa Rais amebadilisha sheria ya madini ili kuwanufaisha watanzania badala ya wageni ,hapa leo tumekuja kuangalia kwa macho ili tufanye uamuzi sahihi …siwezi kumiambia mchimbe sasa hivi ila tutaleta wataalamu wetu wa GST,maliasili na mazingira kwa pamoja ili waje kuona uwezekano wa kupewa eneo la kuchimba ikiwa hapa au kwengine”alisema.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko,( mwenye Tshit nyekundu) na Mbunge wa Mheza Balozi Rajab Adad (mbele) wakielekea eneo lililokuwa likitumiwa na wachimbaji wadogo kuchimba madini pia likidaiwa kuwa chanzo cha maji katika hifadhi ya misitu wa asili wa amani, mheza Tanga. 
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko,( katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Sakale, Mheza mkoani Tanga, waliokuwa wakiomba kuruhusiwa kufanya shughuli za uchimbaji madini katika eneo linalodaiwa kuwa ni chanzo cha maji yanayotumika Mkoa wa Tanga.
Hivyo makala WATAALAM KUCHUNGUNZA UCHIMBAJI MADINI HIFADHI YA AMANI, TANGA
yaani makala yote WATAALAM KUCHUNGUNZA UCHIMBAJI MADINI HIFADHI YA AMANI, TANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATAALAM KUCHUNGUNZA UCHIMBAJI MADINI HIFADHI YA AMANI, TANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/wataalam-kuchungunza-uchimbaji-madini.html
0 Response to "WATAALAM KUCHUNGUNZA UCHIMBAJI MADINI HIFADHI YA AMANI, TANGA"
Post a Comment