Loading...

WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO

Loading...
WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO
link : WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO

soma pia


WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wanaoshiriki kozi fupi ya tano ya viongozi wahakikishe watakaporudi kwenye maeneo yao ya utendaji wawe wamebadilika kimtazamo, kihoja, kiushauri pamoja na utoaji maamuzi.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Agosti 13, 2018) wakati akifungua kozi ya tano ya muda mfupi ya viongozi inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema chuo hicho kilianzishwa kwa lengo la kulisaidia Taifa kujenga uwezo wa viongozi ili wanaohitimu mafunzo hayo wawe na uchambuzi wa kina na wa kimkakati ili kuweza kutatua mambo mbalimbali ya usalama wa Taifa na matatizo yanayotakiwa kushughulikiwa kimkakati.

“Chuo hiki kilianzishwa ili kuwaleta washiriki kutoka taasisi zote za Serikali na sekta binafsi waweze kujadili mambo mbalimbali ya kimkakati ili wanapokuwa wanatekeleza wajibu wao watambue kuwa ni kwa kiasi gani matokeo ya maamuzi yao yataathiri mambo ya kijamii, kiuchumi, uhusiano wa kidiplomasia na siasa za ndani kwa ujumla wake”.

Amesema ushirikiano kuhusu kutatua matatizo uanze wakati wa mafunzo hayo na uendelee hata hapo baadaye watakaporejea kwenye maeneo yao ya kazi. “Sisi viongozi wenu tunatarajia kuona kuwa mtakapohitimu mafunzo haya mtakuwa mmebadilika kimtizamo na kwamba taasisi zenu zitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza lugha moja”.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13.2018 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, akizungumza na washiriki, kwenye ufunguzi wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13.2018.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, akizungumza na washiriki, kwenye ufunguzi wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, Agosti 13.2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya tai, kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, baada ya kufungua kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13.2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya peni, kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, baada ya kufungua kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13. 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13.2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme, baada ya ufunguzi wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam, Agosti 13.2018, katikati ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo, baada ya ufunguzi wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam, Agosti 13.2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO

yaani makala yote WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/waziri-mkuu-awataka-viongozi-wabadilike_13.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO"

Post a Comment

Loading...