Loading...
title : WETENDAJI WA AFYA WAPEWA ONYO.
link : WETENDAJI WA AFYA WAPEWA ONYO.
WETENDAJI WA AFYA WAPEWA ONYO.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid.
Mwamba wa habari.
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed amewakumbusha watendaji wa wizara hiyo kuwa huduma za matibabu ikiwemo ya afya kwa wanawake na watoto zinatolewa bure.
Amesema kuwa serikali haitamvumilia mtendaji ambaye atawatoza fedha wananchi kwa ajili ya kupata huduma za afya ikiwemo dawa ambazo zipo.
Hamad alisema hayo wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Kituo cha Afya cha Fuoni ambapo hivi karibuni wananchi wakiwemo wajawazito walitoa malalamiko ya kutozwa fedha kwa ajili ya baadhi ya vipimo.
Alisema huduma za upimaji kwa wajawazito na watoto zinatolewa bure, ambapo katika bajeti ya Wizara ya Afya mwaka wa fedha 2018-2019 serikali imeongeza bajeti ya huduma za afya.
Alisema kwamba lengo la kuongeza bajeti ni kuwawezesha wananchi ikiwemo wajawazito na watoto kupata huduma hizo bure.
"Nasisitiza tena ni marufuku kwa watendaji wa Wizara ya Afya kuwatoza fedha wananchi ikiwemo wajawazito wanaokuja hapa kwa ajili ya kupima afya zao, Rais Shein(Ali Mohamed) amekataza kabisa suala la kutoza fedha wananchi na ndiyo maana bajeti ya afya imeongezwa,’’alisema.
Aidha amewataka watendaji katika bohari kuu kuwasilisha orodha ya mahitaji yao mapema ili waweze kuingizwa katika orodha ya kupata dawa zinazohitajika.
‘’Tuna dawa za kutosha, tatizo lipo kwa watendaji wanachelewesha kuwasilisha mahitaji ya dawa katika vituo vya afya,’’alisema.
Daktari wa Wilaya ya Mjini Magharibi l, Rahma Maisara alisema watahakikisha hakuna tatizo la upungufu wa dawa zinazohitajika kwa wananchi ikiwemo mahitaji ya wajawazito na vipimo vyake. aliwakumbusha watendaji wa Kituo cha Afya cha Fuoni na vituo vingine kwamba huduma za afya zinatolewa bure na hakuna sababu ya mwananchi kutozwa fedha kwa ajili ya kupata matibabu.
"Katika Kituo cha Afya cha Fuoni tutahakikisha hakuna mgonjwa atakayetozwa fedha kwa ajili ya kupata huduma za afya ikiwemo vipimo kwa wajawazito,’’alisema.
Hivyo makala WETENDAJI WA AFYA WAPEWA ONYO.
yaani makala yote WETENDAJI WA AFYA WAPEWA ONYO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WETENDAJI WA AFYA WAPEWA ONYO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/wetendaji-wa-afya-wapewa-onyo.html
0 Response to "WETENDAJI WA AFYA WAPEWA ONYO."
Post a Comment