Loading...
title : 30 WAITWA STARS MKUDE,KAPOMBE,BOCCO NDANI
link : 30 WAITWA STARS MKUDE,KAPOMBE,BOCCO NDANI
30 WAITWA STARS MKUDE,KAPOMBE,BOCCO NDANI
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa stars', Emmanuel Amunike akizungumza na waandishi wa habari jijni Dar es Salaam leo. katikati kushoto ni Afisa habari habari na mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Criford Ndimbo kulia ni Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa stars'.
Na Agness Francis,Globu ya jamii.
KATIKA kuelekea mtanange wa kufuzu Afcon 2019 dhidi ya cape Verde Oktoba 12 na 16 mwaka huu,kocha mkuu wa Taifa stars Emanuel Amuike ametangaza rasmi kikosi cha wachezaji 30 watakaoingia kambini.
Wachezaji watakao ikingia kambini itakayoanza septemba 30 mwaka huu ni walinda Mlango namba 1 Aishi Manula wa kikosi cha Simba, 2 Beno kakolanya Yanga pamoja na Mohamed Abdalah wa JKT Tanzania.
Walinzi ni Hassani Kessy (Nkana),Shomari Kapombe (Simba),Salum Kimenya (Prisons),Gadiel Michael (Yanga), Paul Ngalema (Lipuli),Aggrey Morris (Azam),David Mwantika (Azam),Abdalah Kheri (Azam),Kelvin Yondani (Yanga),Andre Vicent (Yanga) pamoja na Abdi Banda wa Baroka fc.
Viungo wakiwa ni Himidi Mao (Petro Jet),Simon Msuva (El Jadida),Mudathir Yahya (Azam),Frank Domayo (Azam),Jonas Mkude (Simba),Feisal Salum (Yanga),Salum Kihimbwa (Mtibwa sugar) na Farid Mussa wa Tenerife.
Huku washambuliaji wa kikosi hicho atakuwa Mbwana Samantha (KRC Gank),Tomas Ulimwengu (Al hilal),John Bcco (Simba),Yahya Zayd (BDFXL),Kelvin Sabah (Mtibwa sugar) na Shaban Iddy Chilunda (TEXARIFE).
Mchezo huo utakaoanza kupigwa nchini Cape Verde octoba 12 ambapo marudiano yatafanyika Jijini Dar as Salaam katika uwanja wa taifa tarehe 16 mwezi huo.
Michezo iliopita Taifa stats walilazimika kutoa sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Uganda Uganda the Cranes,vile vile pia walifungana mabao 1-1 dhidi Lesotho katika dimba la Azam complex Chamazi.
Taifa stars wakiwa nafasi ya 3 na pointi 2,akifatiwa na Cape Verde wenye alama 1,huku Uganda wakiwa vinara wao kwa pointi 4 katika kundi hilo L.
Mashindano hayo ya Afcon yanatarajia kufayika nchini Camerron mwakani.
Hivyo makala 30 WAITWA STARS MKUDE,KAPOMBE,BOCCO NDANI
yaani makala yote 30 WAITWA STARS MKUDE,KAPOMBE,BOCCO NDANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala 30 WAITWA STARS MKUDE,KAPOMBE,BOCCO NDANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/30-waitwa-stars-mkudekapombebocco-ndani.html
0 Response to "30 WAITWA STARS MKUDE,KAPOMBE,BOCCO NDANI"
Post a Comment