Loading...
title : AJALI: WATU 11 WAPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA
link : AJALI: WATU 11 WAPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA
AJALI: WATU 11 WAPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA
Na Emanuel Madafa- Fadhiri Atick Globu ya Jamii, MBEYA.
WATU 11 wahofiwa kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari manne ikiwemo gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace iliyotokea eneo la Mlima Igawilo Kasoko Jijini hapa.
Kwa majibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa kumi na moja za jioni ambapo chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni kufeli kwa Lory lenye namba T334 DJN lililokuwa limebaba ndizi likitokea Wilayani Rungwe.
Amesema, hadi sasa taarifa waliyoipata ni kwamba vifo vya watu ni 11 na idadi ya majeruhi bado haijapatikana kwani watu waliokuwepo kwenye magari hayo walikimbizwa hospital kwa ajili ya matibabu.
“Kwa sasa taarifa tuliyonayo ni kwamba vifo ni watu watano idadi ya majeruhi bado haijajulikana kwani asilimia kubwa wamekimbizwa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa matibabu, hivyo tunategemea taarifa ya hospitali ili kupata ripoti sahihi ya vifo na majeruhi,”alisema.
Aidha amesema baada ya Lory namba T334 DJN likitokea Tukuyu, kufeli breck hivyo kugonga Dogo ya abiria Hiace namba T883 ABS ambalo nalo liligonga Lory lingine lililopakia ndizi nalo kugonga Lory la mafuta. Amesema , majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajli ya matibabu huku miili ya marehemu watano imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti katika hospitali hiyo.
Baadhi wa mashuhuda wa ajali hiyo, walisema kuwa dereva wa lory lililosababisha ajali alifanya makosa kwani alipoona gari hilo limeferi brek alikuwa na uwezo wa kulichepusha pembeni ili kuepusha ajali hiyo ambayo ni kubwa.
“Dereva alikuwa anakuja mwendokasi alipofika kwenye mteremko huu wa mlima Igawilo ndipo aliposhtuka na kuanza kuingiza gia ambazo zilifeli na kusababisha gari kuserereka lakini alikuwa na uwezo wa kuliegesha gari hili pembeni,”alisema Jamali Ismaili.
Hata hivyo Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya ilifika eneo la tukio.
Hivyo makala AJALI: WATU 11 WAPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA
yaani makala yote AJALI: WATU 11 WAPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AJALI: WATU 11 WAPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/ajali-watu-11-wapoteza-maisha-jijini.html
0 Response to "AJALI: WATU 11 WAPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA"
Post a Comment