Loading...
title : CCM YAAMUA KUWEKA HADHARANI SABABU ZA KUSHINDA UKONGA, MONDULI
link : CCM YAAMUA KUWEKA HADHARANI SABABU ZA KUSHINDA UKONGA, MONDULI
CCM YAAMUA KUWEKA HADHARANI SABABU ZA KUSHINDA UKONGA, MONDULI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewashukuru Watanzania kwa namna ambavyo wameendelea kukiamini huku kikieleza mambo makubwa yanayofanywa na Rais Dk.John Magufuli watu wanaona na ndio siri ya ushindi wao.
Pia kimetangaza kwamba kuanzia mwaka huu vijana wenye kuanzia umri wa miaka 18 hadi miaka 35 watapatiwa elimu ya ufundi bure na hiyo ni fursa kwa vijana.Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Humphrey Polepole wakati anatoa sababu za ushindi wa kishindo ambao Chama hicho wameupata katika uchaguzi mdogo jimbo la Ukonga ,Monduli pamoja na Kata zote ambazo uchaguzi mdogo umefanyika.
Kuhusu kuaminiwa Polepole amesema kutokana na mambo makubwa ambayo yanafanywa na Serikali ya CCM chini ya Rais Dk.John Magufuli wananchi wanaona na ndio maana kimeendelea kuaminika na kupata ushindi wa kishindo"Yanayofanyika ndani ya nchi yetu watu wanaona.Tumeshinda Jimbo la Ukonga na Monduli.Tumeshinda Kata 23 na kati ya hizo 12 tumepita bila kupingwa.
"Siri ya kuendelea kuaminika na kushinda chaguzi ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya CCM chini ya uongozi madhubuti wa Rais.Dk.John Magufuli," amesema Polepole.Amefafanua kwamba unapozungumzia kupita bila kupingwa kuna sababu mbalimbali na kwamba uchaguzi unasimamiwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria na hasa sheria za uchaguzi.
"Hivyo wanaoshiriki chaguzi wanatakiwa kuzingatia sheria na taratibu za uchaguzi na kinyume na hapo unapoteza sifa," amesema.Akifafanua zaidi kuwa wanaojiita wapinzani kwa sasa wamebaki na siasa za kubeza mazuri yanayofanyika.Polepole ameeleza pamoja na mambo makubwa yanayofanyika ya kimaendeleo CCM pia imetoa maagizo na maelekezo kwa mawaziri kushughulika na shida za Watanzania.nakwamba ni marufuku kwa viongozi kujifungia maofisini badala yake watoke kwenda kutatua kero za watu huko waliko.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
Hivyo makala CCM YAAMUA KUWEKA HADHARANI SABABU ZA KUSHINDA UKONGA, MONDULI
yaani makala yote CCM YAAMUA KUWEKA HADHARANI SABABU ZA KUSHINDA UKONGA, MONDULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM YAAMUA KUWEKA HADHARANI SABABU ZA KUSHINDA UKONGA, MONDULI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/ccm-yaamua-kuweka-hadharani-sababu-za.html
0 Response to "CCM YAAMUA KUWEKA HADHARANI SABABU ZA KUSHINDA UKONGA, MONDULI"
Post a Comment