Loading...
title : DC Mjema AWATAKA VIONGOZI WANGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KUENDANA NA KASI YA AWAMU YA TANO.
link : DC Mjema AWATAKA VIONGOZI WANGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KUENDANA NA KASI YA AWAMU YA TANO.
DC Mjema AWATAKA VIONGOZI WANGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KUENDANA NA KASI YA AWAMU YA TANO.
Mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema kuwepo kwa kero nyingi mtaani zisizotatulika ni kikwazo cha cha maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Tabata wakiwa katika eneo la mkutano viwanja vya Tabata shule ya msingi wakiwa tayari kusikiliza mkuu wa wilya ya Ilala Mhe Sophia Mjema.
Amesema lengo la Ziara hiyo ni kutatua kero zinazowakabili wananchi na kwamba tangu kuanza kuwa kwa Ziara hiyo amekutana na changamoto nyingi ambazo zinatokana na kutowajibika kwa Watendaji wa ngazi ya chini.
" Viongozi nawaomba mtatue hizo kero ili kuendana na Kasi ya Mhe.Rais Magufu ya kufanya kazi kwani hapa kazi tu na kuweza kuendana na Ilani ya Chama inatutaka tufanye kazi za kuwasikiliza Wananchi " Amesema DC Mjema.
Katika hatua nyingine amewataka watendaji kufanya vikao angalau Mara moja kwa mwezi ili yeye akiwa katika ziara zake akutane na Kero za maendeleo tu na zile ndogo ziwe zimetatuliwa na Watendaji hao.
Kuhusu kutokukamilika kwa baadhi ya miradi, amesema wale wakandarasi waliopewa Pesa za Serikali na Manispaa kama hawajamaliza miradi kwa wakati watamalizia kwa Pesa zao na kuwataka kukamilisha kwa wakati ili kuupunguza changamoto zinazowakabili wananchi.
Katika hatua nyingine, amesema tatizo la kuchelewa uzoaji wa taka taka , Tabata, ni kutokana na uzembe wa mkandarasi kutokufanya kazi kwa usahihi na kuahidi kuondoka nae ili kujidhihirisha kama amekidhi vigezo na kama hajakizi atamchukulia hatua.
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Tabata Patick Asenga, amemuomba Dc Mjema, kuwasaidia ukarabati wa Shule za Msingi Tatu, Tabata shule, Shule ya Jaica pamoja na Shule ya Mtambani.
" Mkuu wa wilaya mpaka sasa nimetumia Shilingi Milioni 3 na Laki 8 kwa ajili ya ukarabati hivyo bado shule mbili tunaomba msaada wako ili tuweze kufanya ukarabati wa Shule hizi.Amesema Diwani Asenga.
Amesema Mtaa wa Msimbazi mama kwenda Msimbazi Magharibi barabara haipitiki hivyo amemshukuru ujio wa Mkuu huyo wa Wilaya kwani itasaidia kutatua changamoto hiyo.
Ameongeza kuwa Kero nyingine kubwa ni pamoja Daraja la Treni lililopo katika kata hiyo, hakuna barabara ya wapitia kwa miguu jambo linalisababisha vifo vya watu kugongwa na treni hivyo ameomba Kero hiyo kutatuliwa.
Hivyo makala DC Mjema AWATAKA VIONGOZI WANGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KUENDANA NA KASI YA AWAMU YA TANO.
yaani makala yote DC Mjema AWATAKA VIONGOZI WANGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KUENDANA NA KASI YA AWAMU YA TANO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC Mjema AWATAKA VIONGOZI WANGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KUENDANA NA KASI YA AWAMU YA TANO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/dc-mjema-awataka-viongozi-wangazi-za.html
0 Response to "DC Mjema AWATAKA VIONGOZI WANGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KUENDANA NA KASI YA AWAMU YA TANO."
Post a Comment