Loading...

DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER

Loading...
DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER
link : DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER

soma pia


DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER


Na Khadija Seif,Globu ya jamii

KIMBUNGA cha Chama Cha Mapinduzi(CCM)kimeendelea kuvuma na kusomba wanasiasa wa upinzani ambapo leo kimemsomba Diwani wa Kata ya Mtongani wilayani Temeke Bernard Mwakyembe.

Mwakyembe aliyekuwa Chadema ametangaza leo jijini Dar es Salaam kwamba ameamua kuondoka Chadema na sasa amehamia CCM.Ametaja baadhi ya sababu ambazo zimemfanya ahamie CCM ikiwemo ya kuitwa msaliti kwa sababu tu ya kusifu juhudi za Serikali ya Awamu ya tano katika kuwatumikia Watanzania.

"Kwa juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Magufuli ni vyema kuonesha ushirikiano ili kujenga Tanzania iliyo imara," amesema.Pia amesema Rais amefanya jitihada za kuhakikisha msongamano wa foleni barabarani unamalizika na juzi tu amefungua flyover .Pia amesema Serikali imekuwa mstari wa mbele kuboresha huduma za wananchi ikiwemo sekta ya elimu.Aidha Mwakyembe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amefanya mabadiliko mengi kwenye mji huo ikiwemo suala la usafi katika kila kata.

Pia kuwapa nafasi wanawake wajane na waliotelekezwa na wanaume zao na kuwapa nafasi walemavu waliosoma Kupata ajira serikalini.Hivyo ameona ni jambo la kuungwa mkono kwani hakuna wanaoweza kuleta mabadiliko yote haya lakini wapinzani wamekaa kubeza jitihada za Serikali ya Awamu ya tano

Amesema sababu nyingine ambazo zimempeleka CCM ni serq nzuri za Chama hicho kwani kuna ujamaa na kushirikiana."Hakuna anayeama chama kwenda CCM kwa kununuliwa kama inavotafsiriwa na wengi," mesema.Ametoa rai kwa vyama vya upinzani kuunga mkono juhudi hizo kwani maendeleo yote hayo ni kwa faida ya Watanzania wote si kwa Rais, Mkuu wa Mkoa au kwa CCM peke yake.

Diwani wa Kata ya Mtongani wilaya ya Temeke Bernard Mwakyembe akizungumzana na wanahabari sababu zilimzopelekea kuhamia chama cha Mapinduzi


Hivyo makala DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER

yaani makala yote DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/diwani-wa-chadema-dar-atangaza-kujiunga.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER"

Post a Comment

Loading...