Loading...
title : Dk.Kigwangalla ateta na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William Dar
link : Dk.Kigwangalla ateta na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William Dar
Dk.Kigwangalla ateta na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William Dar
Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William (katikati) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) wakati alipowasili kwenye ofisi ndogo ya wizara hiyo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Sheria na Katiba, Mhe. Profesa Paramagamba Kabudi.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla jana amekutana na kuzungumza na Mjukuu wa Malkia wa
Uingereza, Prince William ambaye yupo nchini kwa ziara ya
siku tatu.
Prince William ambaye aliwasili nchini Septemba 26, 2018
kwa ziara maalum ambapo awali alikutana na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu ya Magogoni Jijini
Dar es Salaam, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na
baadae kupokelewa ofisini kwa Waziri w Maliasili na Utalii,
Dkt. Hamisi Kigwangalla, amesema kuwa amefurahia uwepo
wake hapa nchini hali iliyopelekea kukaa kwa muda huo
tofauti na Nchi zingine ambazo amekaa kwa siku moja.
Prince William ameweza kumtembelea Dk. Kigwangalla
katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo Jijijini Dar es Salaam,
ambapo katika mazungumzo baina ya wawili hao, ikiwemo
suala la kuomba msaada wa kusaidia Sekta ya Utalii.
“Kiukweli tokea kumpokea hapa Nchini alipoingia Septemba
26, Prince William amefurahia ..na nimeweza
kumuomba msaada wa masuala mbalimbali ya kusaidia
Sekta ya Utalii na Uhifadhi wa Nchi yetu kutokana na
yeye kuwa na mapenzi ya kipekee kwenye uhifadhi na pia
anakumbukumbu nzuri na Tanzania kiasi cha kukaa siku
tatuhapa tofauti na nchi zingine alizokaa siku moja”
ameeleza Dkt. Kigwangalla.
Miongoni mwa mambo Waziri Dkt. Kigwangalla aliomba
asaidiwe na Prince William ni pamoja na suala la kukijengea
uwezo kikosi kazi cha kudhibiti ujangili Nchini hii ni
pamojana kusaidia kwenye masuala ya utalaam, zana za
kisasa za kiintelijensia na mafunzo.
Pia Dkt. Kigwangalla alimuomba Prince William kusaidia
kwenye mradi wa kujenga makumbusho tatu za
kuhifadhi meno ya tembo ambapo Wizara inakusudio la
kujenga makumbusho hayo katika Mikoa ya Dodoma,
Arusha na Dar es Salaam.
“lengo la kumuomba atusaidie katika kujenga makumbusho
ya kuhifadhi meno ya tembo ni kutokana na Tanzania kuwa
miongoni mwa nchi za awali tano za Afrika kusaini mpango
wa kulinda tembo kule nchini uingereza mwaka 2008.
Ambapo katika progam hiyo, nchi zote ambazo zimesaini,
zinajifunga kwa kufanya meno hayo ya tembo yasiweze
kutumika tena kibiashara na kiuchumi kwa maana ya
kwamba meno hayo hayawezi kuuzwa tena kwa faida za
kiuchumi hivyo na sisi tumeamua kuyalinda na kuyahifadhi
ili iwe ukumbusho vizazi na vizazi tofauti na nchi zingine
ambazo wao waliamua kuziteketeza kwa kuzichoma moto”
alieleza Dkt. Kigwangalla.
Aidha, Dkt. Kigwangalla alimuomba Prince William msaada
mwingine wa ndege aina ya Helkopta Nne, ikiwemo mbili
zitakazokuwa kwa ajili ya dharura na mbili zingine kwa ajili
ya doria kwenye baadhi ya maeneo ya uhifadhi nchini.
Prince William na ujumbe wake huo umeweza kutembelea
Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na pia Chuo cha Wanyamapori
cha Mweka (College of African Wildlife Management, Mweka
(CAWM), kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro na baada ya
hapo ataendelea na ziara yake Nchini Kenya.
Lengo kuu la ziara hiyo ya Prince William ni pamoja na
kufuatilia juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa
wanyama ikiwemo tembo.
Hivyo makala Dk.Kigwangalla ateta na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William Dar
yaani makala yote Dk.Kigwangalla ateta na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William Dar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dk.Kigwangalla ateta na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William Dar mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/dkkigwangalla-ateta-na-mjukuu-wa-malkia.html
0 Response to "Dk.Kigwangalla ateta na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William Dar"
Post a Comment