Loading...
title : Halmashauri ya Kishapu yajipanga kufanya vizuri ukusanyaji mapato
link : Halmashauri ya Kishapu yajipanga kufanya vizuri ukusanyaji mapato
Halmashauri ya Kishapu yajipanga kufanya vizuri ukusanyaji mapato
Na Robert Hokororo, Kishapu.
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imejipanga kufanya vizuri katika ukusanyaji mapato ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 14, 2018 na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Boniphace Butondo wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa za robo ya nne ya mwaka 2017/2018.
Alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia kwa wataalamu wake imeweka mikakati thabiti kuhakikisha inafika maeneo yote na kukusanya mapato kutoka vyanzo vyake mbalimbali.
“Zipo dalili za kufanya vizuri katika ukusanyaji katika mwaka huu mpya wa fedha ingawa bado kuna changamoto nyingi zinatukabili nawaomba wataalamu msikate tamaa tuendelee kuchapa kazi ili tuwahudumie wananchi,” alisisitiza.
Mhe. Butondo ambaye pia ni diwani wa kata ya Lagana aliwataka madiwani kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo zikiwemo ujenzi wa miundombinu mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu iliweza kukusanya kiasi cha sh. Bilioni 25.1 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Bonophace Butondo akifungua kikao cha Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za robo ya nne ya mwaka wa fedha 2017/2018.
Wajumbe wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Hivyo makala Halmashauri ya Kishapu yajipanga kufanya vizuri ukusanyaji mapato
yaani makala yote Halmashauri ya Kishapu yajipanga kufanya vizuri ukusanyaji mapato Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Halmashauri ya Kishapu yajipanga kufanya vizuri ukusanyaji mapato mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/halmashauri-ya-kishapu-yajipanga.html
0 Response to "Halmashauri ya Kishapu yajipanga kufanya vizuri ukusanyaji mapato"
Post a Comment