Loading...
title : IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKIA 44, WATU WALIO HAI 37 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE KATIKA ZIWA VICTORIA
link : IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKIA 44, WATU WALIO HAI 37 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE KATIKA ZIWA VICTORIA
IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKIA 44, WATU WALIO HAI 37 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE KATIKA ZIWA VICTORIA
Na Said Mwishehe,Globu ya kamii
IMEELEZWA kuwa hadi sasa jumla ya miili ya maiti ya watu 44 imetolewa ndani ya maji ya Ziwa Victoria huku pia watu waliokuwa hai 37 wameokolewa baada ya kutokea ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani y
Ukerewe mkoani Mwanza.
Hata hivyo juhudi za kuendelea kuokoa watu waliokuwa ndani ya kivuko hicho ambacho kilizama ziwani jana mchana zinaendelea huku vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wadau wengine wa ukoaji wakiendelea kufanya jitihada za kutafuta miili na watu waliomo ndani ya kivuko hicho.
Akizungumza asubuhi kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ameiambia Michuzi Blog kwamba wanaendelea nq juhudi za kuokoa watu waliokuwa wanasafiri na kivuko hicho na kazi inakwenda vizuri.
Alipoulizwa idadi ya watu ambao wamefainikiwa kuokolewa hadi sasa wakiwa hai amejibu idadi yao imefikia watu 37 na juhudi zinaendelea.
Kuhusu watu waliokufa kutokana na ajali hiyo ,Kamanda amejibu kuwa wamefanikiwa kupata miili ya watu 44.
Hata hivyo alipoulizwa kuhusu idadi ya watu waliokuwa wakisafiri na kivuko hicho ambacho kimepata ajali ,amejibu kwamba kwa sasa ni ngumu kupata idadi yao na kikubwa ambacho wanaendelea nacho ni kuendelea na ukoaji ambalo ndilo muhimu kwa sasa."Tunaendelea na ukoaji wa watu ambao wamezama ,hivyo suala la idadi ya watu tuliweke kando.Tunachoweza kueleza tunaendelea na ukoaji ikiwamo kuwaondoa watu waliokuwa ndani ya meli(kivuko).
Hata hivyo wakati Kamanda akielezea kinachoendelea ikiwemo juhudi za ukoaji,baadhi ya mashuhuda wamedai kivuko hicho kilikuwa na idadi kubwa ya watu pamoja na mizigo.Imedaiwa kuwa idadi ya watu ndani ya kivuko ni zaidi ya 150 huku wengine wakidai walikuwa watu zaidi ya 200.Mbali ya idadi ya watu pia kulikuwa na mizigo mingi hali iliyosababisha kivuko kuzidiwa na kuelemea upande mmoja.
Kivuko cha Mv.Nyerere kabla ya kuzama ziwani inaelezwa kiliondoka Bugorora kwenda Ukara kati ya saa 6 na saa 7.30 mchana na kilizama dakika kama 5 kabla ya kufika kwenye ghati ya Ukara.
Michuzi Blog itaendelea kukujuza kila kinachoendelea katika shughuli za uokoaji.Pia inaungana na Watanzania wote katika kutoa pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wananchi wa Mkoa Mwanza ,ndugu,jamaa na marafiki kutokana na tukio hilo ambalo limesababisha kupoteza roho za Watanzania wenzetu.
Juhudi za uokoaji zilipokuwa zikifanyika hapo jana kufuatia Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani ya Ukerewe mkoani Mwanza kuzama.
Hivyo makala IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKIA 44, WATU WALIO HAI 37 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE KATIKA ZIWA VICTORIA
yaani makala yote IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKIA 44, WATU WALIO HAI 37 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE KATIKA ZIWA VICTORIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKIA 44, WATU WALIO HAI 37 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE KATIKA ZIWA VICTORIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/idadi-ya-miili-iliyoopolewa-yafikia-44.html
0 Response to "IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKIA 44, WATU WALIO HAI 37 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE KATIKA ZIWA VICTORIA"
Post a Comment