Loading...

Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP

Loading...
Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP
link : Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP

soma pia


Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya  Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia(Tazama), Samwel Nyakirang'ani na wenzake, umeieleza mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa (DPP), kwa ajili ya kulipitia na kulifanyia uchambuzi.

Imedaiwa, DPP analichambua kwa ajili ya kuangalia washtakiwa gani washtakiwe na washtakiwa gani waachiwe huru.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Patrick Mwita, ameeleza hayo leo Septemba 19, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai, amewasiliana na wenzake na  wamemueleza kuwa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha uchambuzi, akaiomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi tarehe nyingine

Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja za pande zote , aliutaka upande wa mashtaka kuharakisha zoezi la uchambuzi ili haki iweze kupatikana.

kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 3, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa na kuangalia kama uchambuzi huo umekamilika.

washtakiwa  wengine katika kesi  hiyo ni Nyangi Mataro mwalimu wa shule ya msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.

Mfanyabaishara, Farijia Ahmed mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias, mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus, mkazi wa Soko Maziwa,  Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko, mkazi wa Tungi Kasirati na Henry Fredrick, mkazi wa Tungi Kigamboni.

Wengine ni Audai Ismail ambaye ni mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa  kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, kinyume cha sheria  ya Uhujumu uchumi.

Inadaiwa, kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 huko Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa kwa pamoja walijiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoa katika bomba lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Bandari nchini(TPA).

Pia wanadaiwa  kutoboa  bomba  hilo ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta,  mali ya (TPA).

Aidha wanadaiwa kuharibu  bomba la mafuta mazito lenye upana wa Inchi 28, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi, mali ya (TPA).


Hivyo makala Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP

yaani makala yote Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/jalada-la-kesi-ya-uhujumu-uchumi-dhidi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP"

Post a Comment

Loading...