Loading...

Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika

Loading...
Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika
link : Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika

soma pia


Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika

Hii ni kufuatia huduma za ndege kupitia Jumia kukua kwa 400% ndani ya Julai 2017 na Julai 2018.

Katika kuadhimisha siku ya Utalii Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Septemba 27 ya kila mwaka, Jumia imejitanua tena katika huduma za ndege, safari hii ni kupitia ushirikiano baina yake na Amadeus, kampuni inayoongoza kwa teknolojia za usafiri duniani. Ushirikiano huu ni msingi wa soko jipya la huduma za ndege kwenye mtandao wa Jumia, ikiwa ni hatua nyingine mbele katika kufanya huduma za usafiri barani Afrika kuwa rahisi na nafuu.

Jukwaa hili linalenga kuwawezesha mawakala wa usafiri, ndege, na tovuti za usafiri kuleta masuala yote yahusuyo huduma za ndege mtandaoni, kwa kuwapatia wateja bei nzuri za huduma za ndege zinazopatikana. Takwimu za sasa zinaonyesha kwamba 90% ya soko la huduma za ndege bado liko nje ya mtandaoni wakati ni 10% tu ndiyo lipo mtandaoni. Hii inakuja kufuatia kuongezeka kwa wateja wa huduma za ndege kupitia Jumia, ikiwa imeongezeka kwa kasi mpaka kufikia 400% ndani ya kipindi cha Julai 2017 na Julai 2018.

“Jumia inaendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika bidhaa zenye ubunifu kwa wasafiri na watoa huduma za ndege ambazo zitawasaidia kufanya mapinduzi kwenye uendeshaji wa shughuli zao na kuongeza mapato,” anasema Kijanga Geofrey, Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia. “Tunalielewa soko na tunayashughulikia mahitaji yake. Jukwaa lenye ushindani litawaunganisha kwa pamoja watoa maudhui wote kutoa viwango vya chini na tozo ndogo ili kukidhi kuongezeka kwa mahitaji ya wasafiri kupata huduma bora zaidi kwa gharama nafuu,” anaongezea.

Soko pia litatoa uchambuzi wa taarifa ambazo watoaji huduma wa tiketi za ndege wanaweza kuzitumia kutambua fursa mpya, njia na kuwasaidia kutengeneza vifurushi vya wateja wa ndege wanaowalenga.


Hivyo makala Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika

yaani makala yote Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/jumia-na-amadeus-zashirikiana-kuzindua.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika"

Post a Comment

Loading...