Loading...
title : LHRC YASHEREKEA MIAKA 23, WABAINISHA MBIVU MBISHI KATIKA UTENDAJI WAO..
link : LHRC YASHEREKEA MIAKA 23, WABAINISHA MBIVU MBISHI KATIKA UTENDAJI WAO..
LHRC YASHEREKEA MIAKA 23, WABAINISHA MBIVU MBISHI KATIKA UTENDAJI WAO..
Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga akiwa katikati akikata keki leo jijini Dar es Salaam wakati wakiadhimisha miaka 23 ya Kituo hicho tangu kuanzishwa kwake.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa jamii, Asasi za Kiraia, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na taasisi za serikali kuendelea kukuza na kulinda haki za binadamu nchini.
Wito huo umetolewa leo ambapo LHRC imeadhimisha miaka 23 tangu kuanzishwa kwake Septemba 26 I995 na wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga, amesema kuwa siku ya leo wanafuraha kubwa ya kuadhimisha miaka 23 katika kupigania na kutetea haki za binadamu.
Henga amesema kuwa miaka 23 ya kutetea haki za binadamu, LHRC kinajivunia kwa kuwajengea watanzania uwezo juu ya sheria na haki za binadamu.
Amesema kuwa katika kufanikisha wanawafikia watanzania wote wameweza kuwajengea uwezo wasaidizi wa sheria zaidi ya 900 katika wilaya 30 za Tanzania bara kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu.
"Kituo kimefanikiwa kuanzisha mfumo wa uangalizi wa haki za binadamu katika wilaya zote nchini ikiwa na wangalizi I69 waliopo mikoa yote nchini" amesema Henga.
Miongoni mwa mafanikio katika kipindi cha miaka 23 ya LHRC ni pamoja na
I, Kuwa chachu ya mabadiliko ya sera na kutungwa kwa sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya msaada wa kisheria ya mwaka 20I7 pamoja na kanuni zake za mwaka 20I8, ambayo inawatambua wasaidizi wa kisheria waliojengewa uwezo.
II, Kuratibu mtandao wa waangalizi wa uchaguzi Tanzania (TACCEO) na kutoa taarifa ya uangalizi wa uchaguzi mkuu na uchaguzi ndogo za marudio.
iii, Kuibua mambo mbalimbali yaliyopelekea uwajibikaji katika ulinzi wa rasilimali za nchi ikiwemo kupelekea kutungwa kwa sheria za ulinzi wa rasilimali za Nchi ya mwaka 20I7.
iv, Kuanzisha vilabu 27 vya haki za binadamu katika shule za sekondari na vyuo vikuu nchini kwa lengo la kuwajengea vijana uwezo kuhusu sheria na haki za binadamu.
v, Kutoa Msaada kwa wananchi wasio na uwezo wa kufikia huduma za haki kwa kutoa msaada wa kisheria.
vi, Kituo kimeweza kuendesha kesi mbalimbali za kimkakati kwa kushirikiana na wadau tofauti kwa ajili ya kubadilisha sheria na sera ikiwemo kesi ya mgombea binafsi katika mahakama ya Afrika, kesi ya maoni kikatiba pamoja na kesi ya kutetea watu wenye ulemavu.
Hata hivyo miongoni mwa changamoto ambazo zimekuwa kikwanzo katika utendaji wa LHRC ni pamoja na tukio la jeshi la polisi kuvamia kituo cha uangalizi wa uchaguzi mwaka 20I5 na kuwakamata maafisa wa Kituo hicho.
Katika tukio hilo jeshi la polisi walikama simu pamoja na kompyuta 25 zilizokuwa zikitumika kupokea taarifa za uangalizi wa uchaguzi mkuu mwaka 25.
Ameeleza kuwa Tanzania bado kuna uelewa duni wa haki za binadamu miongoni mwa wananchi ambayo hupelekea kutofautisha kazi ya kituo na shughuli za kisiasa au vyama vya siasa.
"Tuna changamoto ya rasilimali watu na fedha ili kukidhi matarajio ya wananchi kutokana watanzania wengi bado wanaitaji msaada wa kisheria" amesema Henga.
Hivyo makala LHRC YASHEREKEA MIAKA 23, WABAINISHA MBIVU MBISHI KATIKA UTENDAJI WAO..
yaani makala yote LHRC YASHEREKEA MIAKA 23, WABAINISHA MBIVU MBISHI KATIKA UTENDAJI WAO.. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LHRC YASHEREKEA MIAKA 23, WABAINISHA MBIVU MBISHI KATIKA UTENDAJI WAO.. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/lhrc-yasherekea-miaka-23-wabainisha.html
0 Response to "LHRC YASHEREKEA MIAKA 23, WABAINISHA MBIVU MBISHI KATIKA UTENDAJI WAO.."
Post a Comment