Loading...
title : MAKONTENA YA RC MAKONDA YAANZA KUPIGWA MNADA BANDARINI DAR
link : MAKONTENA YA RC MAKONDA YAANZA KUPIGWA MNADA BANDARINI DAR
MAKONTENA YA RC MAKONDA YAANZA KUPIGWA MNADA BANDARINI DAR
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
MAKONTENA ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambayo yamebeba samani za walimu yameanza kupigwa mnada.
Hatua ya kupiga mnada makontena hayo inakuja baada ya Rais Dk.John Magufuli kutoa maagizo ya kuhakikisha yanalipiwa kodi na ikishindikana yapigwe mnada.
Rais Dk.Magufuli alitoa kauli hiyo juzi akiwa mkoani Chato na sababu za kutoa ufafanuzi na maelekezo hayo baada ya kuona Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam analazimisha makontena hayo yatolewe bila kulipiwa kodi.
Hivyo leo makontena hayo yameanza kupigwa mnada kuanzia saa tatu ya asubuhi na unafanyika bandari ya Dar es Salaam upande wa Malawi Cargo.
Mnada huo tangu ulipoanza asubuhi unaendelea kufanyika hadi sasa.
Katika mnada huo wananchi, taasisi,mashirika na baadhi ya viongozi wa Serikali wamejitokeza kwa lengo la nununua samani zilizopo kwenye makontena hayo.
Hivyo makala MAKONTENA YA RC MAKONDA YAANZA KUPIGWA MNADA BANDARINI DAR
yaani makala yote MAKONTENA YA RC MAKONDA YAANZA KUPIGWA MNADA BANDARINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONTENA YA RC MAKONDA YAANZA KUPIGWA MNADA BANDARINI DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/makontena-ya-rc-makonda-yaanza-kupigwa.html
0 Response to "MAKONTENA YA RC MAKONDA YAANZA KUPIGWA MNADA BANDARINI DAR"
Post a Comment