Loading...
title : MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI YAZIDI KUONGEZA MAPATO
link : MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI YAZIDI KUONGEZA MAPATO
MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI YAZIDI KUONGEZA MAPATO
Mageuzi makubwa katika sekta ya madini nchini yameifanya sekta hiyo kuendelea kuongeza mapato ya Serikali kutoka bilioni 194.6 ilizopanga kukusanya mwaka 2017/18 hadi kufikia shilingi bilioni 301.6 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 55.
Hayo yameelezwa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi mkoani Geita wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Serikali.
Dkt. Abbasi ameeleza kuwa ongezeko hilo la mapato katika sekta ya madini limechagizwa na mabadilikomkatika sheria za madini, kujengwa kwa ukuta wa Mirerani na kuzuia kwa usafirishaji wa mabaki (kaboni) ya dhahabu nje ya mkoa yanapochimbwa madini.
“Mheshimiwa Rais aliagiza kujengwa ukuta eneo la wachimbaji wadogo la Mirerani na April mwaka huu ukuta huo ulikamilika na kuwezesha kuongezeka kutoka kilo 164.6 za madini ya Tanzanite yenye thamani yas milioni 71.8 mwaka 2016 hadi kufikia kilo 449.6 zenye thamani ya shilingi milioni 893.8 kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2018”, ameeleza Msemaji Mkuu wa Serikali.
Ameeleza kuwa kutokana na usimamizi mzuri, makampuni ya uchimbaji madini yameendelea kutoa mchango wake kwa jamii ambapo Geita Gold Mine imetoa shilingi bilioni 9.2 kwa mkoa wa Geita kama mchango wa kampuni hiyo kwa maendeleo ya mkoa huo.
Aidha, Msemaji Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa zuio la kaboni zenye dhahabu kusafirishwa na kuchakatwa nje ya mkoa zinakozalishwa limesaidia kuongeza pato kwa Serikali kufikia shilingi milioni 850 kwa mwezi Agosti mwaka huu kutoka shilingi milioni 400 kwa mwezi April.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi.
Hivyo makala MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI YAZIDI KUONGEZA MAPATO
yaani makala yote MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI YAZIDI KUONGEZA MAPATO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI YAZIDI KUONGEZA MAPATO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/mapinduzi-makubwa-sekta-ya-madini.html
0 Response to "MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI YAZIDI KUONGEZA MAPATO"
Post a Comment