Loading...

Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma

Loading...
Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma
link : Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma

soma pia


Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde, ameipongeza Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, kwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kujali usalama wa wanafunzi kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya uchoraji kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa huo.Amesema tangu mwaka 2013, kampuni hiyo ilipoanzisha kampeni ya usalama barabarani ambayo imekuwa na lengo la kupunguza ajali za usalama barabani na sasa mafanikio yanaonekana.

“Tangu ilipozinduliwa kampeni hii tunaona kuna mafanikio na katika awamu ya kwanza ya mafunzo haya wanafunzi 9,152, wamepewa mafunzo usalama barabarani ikiwamo kushiriki katika michoro hongereni sana Puma.“….na la kufurahisha zaidi ni hatua ya kuzishirikisha na shule za wanafunzi wenye ulemavu ikiwamo ya shule mojawapo ya Mkoani Ruvuma,” amesema Mavunde.

Awali Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuwaelimisha wanafunzi kuhusu usalama barabarani tangu mwaka 2013 ilipozinduliwa kampeni hiyo.“Tangu ilipoanza kampeni hii tumetoa mafunzo kwa wanafunzi wapatao 68,000 katika shule 63 za mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Geita, Kilimanjaro na Ruvuma,” amesema .
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakiwasaidia kuvuka kwenye kivuko wanafunzi wa shule za msingi za Upanga na Maktaba mara baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakipiga picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa shule za msingi za Upanga na Maktaba mara baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakikabidhi mfano wa cheki yenye tahamani ya shilingi milioni tano kwa mwalimu Mkuu wa wa shule ya msingi Upanga Ailika Yahya mara baada ya shule hiyo kuibuka mshindi katika shindano hilo lililoshirikisha wanafunzi wa shule za msingi za Upanga na Maktaba katika shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde akimkabidhi zawadi za mshindi wa kwanza Mwanafunzi wa shule za msingi ya Maktaba Francisco Salvatory kwa mwakilishi wake Elisha Msafiri katika hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam kushoto ni mwalimu mkuu wa shule ya Upanga Ailika Yahya.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti pamoja na majaji wengine wakichambua picha za wanafunzi walioshinda katika shindano hilo.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>


Hivyo makala Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma

yaani makala yote Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/mavunde-aipongeza-kampuni-ya-mafuta-puma.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma"

Post a Comment

Loading...