Loading...
Loading...
- Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa , tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title :
link :

soma pia


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kutoka kushoto) akifungua mkutano wa wadau wa afya hivi karibuni mkoani humo. Wengine ni  Katibu Tawala Mkoa huo Msalika Makungu( kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala(wa pili kutoka kulia) na  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba(kulia)

NA TIGANYA VINCENT

RS TABORA

19 September 2018

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Mkoa wa Tabora umelipa jumla ya bilioni 3.8 kwa watoa huduma mbalimbali mkoani humo katika mwaka wa fedha uliopita.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Jacob Mwailubi wakati wa mkutano wa wadau wa afya wa Mkoa huo.

Alisema vituo vya Serikali vimelipwa bilioni 1.021 , watoa huduma wa binafsi bilioni 1.246 na Vituo vya Taasisi za dini vimelipwa kiasi bilioni 1.566.

Aidha Mwailubi alisema NHIF mkoani humo imefanikiwa kusajili wanachama wapya 3,063 katika mwaka wa fedha uliopita na kuufanya ufikishe wanachama  20,400.

Mwailubi alisema kati yao watumishi wa umma ni 16,938, Mashirika binafsi 307, wastaafu 175, Vyuo vya Elimu ya juu 2,131, Madiwani 268,Viongozi madhehebu ya dini 125, Wanachama binafsi 6 na Watoto chini ya miaka 18 ni  450.

Aidha alisema katika kipindi hicho Ofisi ya Mkoa ya NHIF iliweza kukusanya jumla ya milioni 645.9 kama michango ya wanachama  ambapo kati yake  milioni 325.3 ni michango toka taasisi za umma wakati milioni 320.6 ilikusanywa kutoka mashirika binafsi.

Hata hivyo alisema Halmashauri za Wilaya ya Tabora –Uyui, Igunga na Urambo hazijalipa malimbikizo ya michango ya Watumishi wanaolipwa kupitia mapato ya ndani ya jumla milioni 39.5.

Mwailubi alisema Halmashauri ya wilaya Tabora  inadaiwa shilingi milioni 1.6, Igunga milioni 28.2 na Urambo milioni 8.6.

Aliwahimiza michango hiyo ilipwe ili watumishi husika wapate huduma za matibabu.

Wakati huo huo Mwailubi alisema NHIF imesajili jumla ya Vituo vya Huduma za Afya  302 ambapo kati ya hivyo  vituo 243  vinavyomilikiwa na serikali, vituo 24 ni Taasisi na mashirika yasio ya serikali na  vituo 35 vinavyomilikiwa na watu binafsi yakiwemo maduka ya dawa.


Hivyo makala

yaani makala yote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/mkuu-wa-mkoa-wa-tabora-aggrey-mwanriwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to " "

Post a Comment

Loading...