Loading...
title : Mtibwa Tff,tafuteni mdhamini mkuu
link : Mtibwa Tff,tafuteni mdhamini mkuu
Mtibwa Tff,tafuteni mdhamini mkuu
Na Tuzo Mapunda
Mwamba wa habari
KLABU ya Mtibwa imelitaka Shirikisho la soka la mpira wa miguu Tff,Kuacha kubweteka na badala yake watafute mdhamini mkuu wa kusimamia Ligi kuu Tanzania Bara.
Ligi hiyo kwa sasa haina mdhamini mkuu baada ya kujitoa Vodacom aliyekuwa mdhamini mkuu wa ligi hiyo kwa misimu iliyopita.
Akizungumza na mwambawahabari.blogspot.com ,Ofisa habari wa klabu hiyo Thobias Kifaru alisema mdhamini mkuu anasaidia kutoa baadhi ya gharama na hiyo kuipa uhuru timu kujiendesha .
“TFF ,isipo chukua hatua za haraka itafikia kipindi timu zitashindwa kusafirisha kikosi kutokana na kukumbwa na ukata.” Alisema Kifaru.
Alisema kwa sasa ligi inaonekana kuwa na ushindani lakini itafika katikati ya msimu ushindani utapungua na kuzipa nafasi timu zenye uwezo kuendelea kupata matokeo.
Kifaru alisema ukweli ni kwamba klabu zetu hapa mchini bado hazijafanya uwekezaji mkubwa na zimekuwa zikimtegemea ,mdhamini mkuu kwa kiasi kikubwa.
Alisema Mtibwa wana bajeti ya miaka 10 hivyo kwa upande wao hawana hofu na kukosekana kwa mdhamini mkuu na wataendelea kupambana kwa nguvu moja ili kuchukua taji la ligi hiyo.
Ligi kuu msimu huu inashirikisha timu 20 tofauti na msimu uliopita ilikuwa inashirikisha timu 16,kitendo cha kukosekana mdhamini huyo nikuzifanya baadhi ya timu kuwa kwenye wakati mgumu hasa kwenye kuwalipa mshara wa chezaji na kuendesha timu.
Hivyo makala Mtibwa Tff,tafuteni mdhamini mkuu
yaani makala yote Mtibwa Tff,tafuteni mdhamini mkuu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mtibwa Tff,tafuteni mdhamini mkuu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/mtibwa-tfftafuteni-mdhamini-mkuu_22.html
0 Response to "Mtibwa Tff,tafuteni mdhamini mkuu"
Post a Comment