Loading...

Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet

Loading...
Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet
link : Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet

soma pia


Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet

 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, Ibrahim Pius Mbwilo (28) ameshinda Sh 239,417,800 kupitia mchezo wa Perfect 12 unaoendeshwa na kampuni ya M-Bet.

Mbwilo ambaye anasoma shahada ya Utawala wa Biashara (Business Administration) akiwa mwaka wa pili, alibashiri kiusahihi mechi 12 za ligi mbalimbali za ulaya. Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi alisema kuwa Mbwilo ambaye ni shabiki wa timu ya Simba na Chelsea ya Uingereza, amekuwa mshindi wa pili kupata fedha nyingi zaidi tokea kuanzishwa kwa droo ya Perfect 12. Mshindi wa kwanza alipata Sh 280 millioni.

Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa na kuwasaidia watanzania kubadili maisha yao kwa kutumia Sh1,000 tu. “Nawaomba Watanzania kuendelea kubashiri kwa kutumia michezo yetu,kuna nafasi kubwa ya kushinda na mpaka sasa tumepata jumla ya washindi 10 ambao wamefaidika na droo yao,” alisema Mushi.

Alisema kuwa Serikali imepata Sh 47 millioni kutokana na kodi kutokana na ushindi huo wa Mbwilo. Akizungumza baada ya kupokea hundi yake, Mbwilo alisema kuwa amefarijika sana kupata fedha hizo ambazo atazitumia kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo, kuwasomesha ndugu zake na kusaidia familia.

Mbwilo alisema kuwa pia atatumia fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza biashara yake ya kuuza matofali na kuanzisha biashara nyingine. Alisema kuwa yeye ni mtoto yatima na aliishi maisha ya mitaani huku akiokota taka na kuziuza kama mbolea (samadi) kwa akina mama ambao walikuwa wateja wake kwa lengo la kumsaidia.

“Niliishi mitaani, nilikwenda jalalani kutafuta matunda, taka, kutafuta taka na kuziuka kama mbolea, nilifanya hivyo baada ya kuachwa na mlezi wangu nikiwa kidato cha pili, naguswa na aina hiyo ya watoto yatima hiyo. “Tarehe 6 mwezi huu, nilitumia sh 1,000 kubashiri na kupata kiasi kikubwa cha fedha, namshukuru Mungu kwani wanaobashiri wengi, nitasaidia kituo cha watoto yatima kwa kunua magodoro, kuna kituo cha watoto yatima ambao hawana vitanda hata magodoro, nitafanya hivyo kwa sababu mimi mwenyewe nimetokea huko,” alisema Mbwilo.

 Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Kulia) akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi wa mchezo wa Perfect 12, Ibrahim Mbwilo (28) ambaye ameshindia Sh milioni 239.4. Mbwilo ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Chuo Kikuu Cha Iringa. Picha: Mpigapicha wetu 


Hivyo makala Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet

yaani makala yote Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/mwanafunzi-chuo-kikuu-iringa-ashinda.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet"

Post a Comment

Loading...