Loading...
title : 'NCHI ZA AFRIKA KUENDELEA KUKABILIWA NA UHABA WA MBEGU BORA ZENYE KUTOA MAZAO MENGI'
link : 'NCHI ZA AFRIKA KUENDELEA KUKABILIWA NA UHABA WA MBEGU BORA ZENYE KUTOA MAZAO MENGI'
'NCHI ZA AFRIKA KUENDELEA KUKABILIWA NA UHABA WA MBEGU BORA ZENYE KUTOA MAZAO MENGI'
Meneja masoko wa kampuni ya kuzalisha mbegu za awali ya Quality Basic Seed, Cliffe ingoi akiwaeleza waandishi wa habari namna kampuni yake inavyofanya uzalishaji wa mbegu hizo.
Seif Mangwangi,Arusha
NCHI za Afrika zitaendelea kukabiliwa na uhaba wa mbegu bora za msingi zenye kutoa mazao mengi na bora kutokana na uzalishaji wa mbegu hizo kuwa mdogo kulinganisha na mahitaji halisi.
Hali hiyo itaendelea kusababisha uzalishaji wa vyakula kuwa wa chini na hivyo kushindwa kukabili tatizo la njaa linalozikumba nchi nyingi barani Afrika mara kwa mara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Meneja Masoko wa Kampuni ya kuzalisha mbegu za msingi ya Quality Basic seed yenye makao yake mkuu nchini Kenya, Wycliffe Ingoi amesema mahitaji ya mbegu bora za msingi ni kilo 156250 kwa mwaka.
Amesema kiwango hicho ni kikubwa kutokana na ugumu wa kuzalisha mbegu hizo sanjari na uwepo wa kampuni chache zinazoweza kuzalisha mbegu hizo.
" Wakulima wamekuwa wakipata mazao machache kutokana na uhaba wa mbegu za msingi na hivyo kulazimika kutumia mbegu zisizo na ubora na ambazo hazijazalishwa kitaalam, sisi kama QBS tumekuja kujaribu kumaliza hili tatizo japo kwa kiasi fulani,"amesema.
Aliziomba Serikali za Afrika kushirikiana na kampuni zinazozalisha mbegu za msingi ili kufanikisha zoezi la kupatikana kwa mbegu bora na zenye kutoa mazao mengi.
kwa upande wake Ofisa Habari wa taasisi ya kilimo ya African Agriculture Technology Foundation (AATF),inayosaidia kusambaz teknolojia ya kilimo Afrika, Everlyne Situma alisema kampuni za mbegu zimekuwa zikishindwa kuzalisha mbegu za kutosha kutokana na ugumu wa kutayarisha mbegu za msingi.
Amesema kampuni ya Quality Basic Seed imekuwa mfano wa kuanzisha utaalam huo na hivyo kuwa msaada kwa kampuni za uzalishaji wa mbegu Afrika.
Hivyo makala 'NCHI ZA AFRIKA KUENDELEA KUKABILIWA NA UHABA WA MBEGU BORA ZENYE KUTOA MAZAO MENGI'
yaani makala yote 'NCHI ZA AFRIKA KUENDELEA KUKABILIWA NA UHABA WA MBEGU BORA ZENYE KUTOA MAZAO MENGI' Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala 'NCHI ZA AFRIKA KUENDELEA KUKABILIWA NA UHABA WA MBEGU BORA ZENYE KUTOA MAZAO MENGI' mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/nchi-za-afrika-kuendelea-kukabiliwa-na.html
0 Response to "'NCHI ZA AFRIKA KUENDELEA KUKABILIWA NA UHABA WA MBEGU BORA ZENYE KUTOA MAZAO MENGI'"
Post a Comment