Loading...

Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja

Loading...
Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja
link : Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja

soma pia


Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja

Na Greyson Mwase, Dodoma
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amemwagiza Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya kuhakikisha wanakipatia kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini kijulikanacho  kwa jina la “Hapa Kazi Tu” kinachoendesha shughuli za uchimbaji wa madini aina ya sunstone katika kijiji cha Suguta wilayani Kongwa mkoani Dodoma leseni ya uchimbaji madini ndani ya mwezi mmoja kwa kufuata kanuni na sheria za madini.

Profesa Kikula alitoa agizo hilo tarehe 05 Septemba, 2018 katika  machimbo ya madini hayo yaliyopo katika kijiji hicho kwenye ziara yake ya siku mbili katika wilaya za Kongwa na Mpwapwa yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji madini zinazofanywa na wachimbaji wadogo, kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili.

Katika ziara hiyo, Profesa Kikula aliambatana na Makamishna wa Tume, Profesa Abdulkarim Mruma na Haroun Kinega, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya pamoja na waandishi wa habari.

Mara baada ya kusikiliza kero za wachimbaji wadogo hao Profesa Kikula mbali na kutoa  agizo hilo alimwelekeza Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto, kuhakikisha anasaidia kikundi cha wachimbaji wadogo hao katika taratibu zote za usajili wa kikundi  kabla ya kuanza kushirikiana na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma katika upatikanaji wa leseni ndani ya mwezi mmoja.

Aidha, Profesa Kikula alimtaka Mwenyekiti huyo kuwasaidia wachimbaji hao katika usajili kwenye vyama vya  wachimbaji madini Tanzania pamoja na utafutaji wa masoko na bei elekezi kwenye masoko ya kimataifa.

“Kutokana na kuwa na mtandao mkubwa na uelewa kwenye masoko na bei elekezi za madini kwenye masoko ya kimataifa, nakuelekeza kama Mwenyekiti wa wachimbaji kuhakikisha unawasaidia wachimbaji hawa hususan kwenye maeneo ya masoko na bei elekezi ili uchimbaji wao uwanufaishe wao na Serikali kupata mapato stahiki,” alisema Profesa Kikula.
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi (kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
 Kutoka kushoto, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya, Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Deogratius Ndejembie na Kamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kikao hicho.
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) na Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma (kulia) wakiangalia moja ya mawe ili kubaini madini yaliyomo kwenye machimbo ya Suguta yaliyopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (mbele) pamoja na msafara wake wakiendelea na ziara kwenye kwenye machimbo ya Suguta yaliyopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Mmoja wa watendaji wa migodi ya shaba ya Rays Metal Corporation na Tambi Minerals Resources iliyopo katika kijiji cha Tambi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati). Kulia ni Kamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega.


Hivyo makala Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja

yaani makala yote Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/prof-kikula-aagiza-kikundi-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja"

Post a Comment

Loading...