Loading...
title : PROFESA LIPUMBA AUCHAMBUA UCHUMI WA TANZANIA.
link : PROFESA LIPUMBA AUCHAMBUA UCHUMI WA TANZANIA.
PROFESA LIPUMBA AUCHAMBUA UCHUMI WA TANZANIA.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Baraza Kuu la Uongozi Taifa Chama Cha Wananchi (CUF) ameitaka kamati ya utendaji Taifa kwa kushirikiana na watafiti wa ndani na nje ya nchi kuandaa mikakati na sera ili kukuza uchumi pamoja na unaongezeka fursa za ajira nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa ni vizuri kujenga taifa la wananchi walio huru kwa kupambana na rushwa na ufisadi.
Profesa Lipumba ni Mchumi amesema kuwa baraza Kuu la CUF linatambua na kuipongeza serikali katika juhudi za kujenga miundombinu ya reli (SGR), barabara, maji, umeme, upanuzi wa bandari pamoja na ujenzi wa bombo la mafuta ambapo ni hatua muhimu katika kuchochea na kukuza uchumi.
"Pamoja na takwimu kuonesha pato la taifa linakua kwa asilimia 7 hali halisi ya maisha ya wananchi ni ngumu, mzunguko wa fedha haukidhi mahitaji" amesema Profesa Lipumba.
Mchumi huyo ameeleza kuwa kasi ya ongezeko la ujazi wa fedha (Money Supply) mwaka 20I6/I7 na 20I7/I8 imekuwa chini kuliko miaka yote tangu Benki Kuu ya Tanzania kuanzishwa mwaka I966.
Profesa Lipumba amefafanua kuwa kiwango cha ukuaji wa mikopo sekta binafsi imeporomoka kutoka asilimia 25 mwaka 20I5 na kufikia asilimia I.7.
Amesema kuwa sekta binafsi haiwezi kuongeza ajira bila kupata mikopo na kusaidia kuekeza na kuendesha biashara jambo ambalo litasaidia kuongeza mzunguko wa fedha katika uchumi.
"Serikali ilipe madeni yake kwa wafanyakazi wa serikali na wafanyabiashara walioiuzia bidhaa na huduma, benki iongeze ukuaji wa ujazi wa fedha pamoja na kupunguza riba ya mikopo" amesema Profesa Lipumba.
Katika hatua nyengine mchumi huyo amesema kuwa mazingira ya kufanya biashara Tanzania sio rafiki kutokana ripoti ya Benki ya dunia ya mazingira ya kufanya biashara (Doing business 20I8) imebainisha Tanzania inashika nafasi ya I37.
Amesema kuwa ripoti inaonyesha kuwa Kenya inashika nafasi ya 80, Rwanda ya 42 kati ya nchi I90.
"Mazingira hasi ya kufanya biashara yanazuia uwekezaji wa sekta binafsi ndani na nje ya nchi, pia uagizaji wa bidhaa toka nje umepunguza dola bilioni I2.7 mwaka 20I4 hadi kufikia dola bilioni 7.8 kwa mwaka 20I7" amesema Profesa Lipumba.
Amesema uwekezaji katika viwanda unategemea uagizaji wa mashine na mitambo kutoka nje ya nchi.
Hivyo makala PROFESA LIPUMBA AUCHAMBUA UCHUMI WA TANZANIA.
yaani makala yote PROFESA LIPUMBA AUCHAMBUA UCHUMI WA TANZANIA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROFESA LIPUMBA AUCHAMBUA UCHUMI WA TANZANIA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/profesa-lipumba-auchambua-uchumi-wa.html
0 Response to "PROFESA LIPUMBA AUCHAMBUA UCHUMI WA TANZANIA."
Post a Comment