Loading...
title : RC MAKONDA AFUTA AIBU YA WALIMU KUCHANGIA CHOO NA WANAFUNZI,UJENZI BARABARA YA GOBA MBIONI KUKAMILIKA.
link : RC MAKONDA AFUTA AIBU YA WALIMU KUCHANGIA CHOO NA WANAFUNZI,UJENZI BARABARA YA GOBA MBIONI KUKAMILIKA.
RC MAKONDA AFUTA AIBU YA WALIMU KUCHANGIA CHOO NA WANAFUNZI,UJENZI BARABARA YA GOBA MBIONI KUKAMILIKA.
Mwamba wa habari
Na John Luhende
Serikali Mkoani Dar es Salaam, imeeleza kuridhishwa na ujenzi bwa miundombinu inayotekelezwa chini ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADs) inayogharimu zaidi y ash.bilioni 37.6
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa barabara zinazojengwa chini ya wakala huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema hatua iliyofikiwa na wakandarasi wanaojenga miundombinu hiyo zikiwemo barabara, madaraja, mitaro na vivuko.Katika ziara hiyo Makonda alikagua barabara ya Wazo hadi Mbenzi Luis ambapo alisema kipande cha Goba –Wazo chenye urefu wa ujenzi wake wa kiwango cha lami utagharimu ya sh.bilioni 9.5. na kwamba mkandarasi kampuni ya Becco yuko eneo la mradi.
“Barabara inayotoka Wazo hadi Mbezi Luis ujenzi unaendelea. Kipande cha kutoka Wazo hadi Goba kinazaidi ya kilomita 10 lakini kutoka Madale kwenda Goba ni kilomita tano mkandarasi yukon kazini na ujenzi utagharimu sh.bilioni 9.5 u jenzi unaenda vizuri na umefikia zaidi ya asilimia 70,”alisema Makonda.“ Kutoka goba hadi Masaba kuna barabara ya urefu bwa kilomita tisa na ujenzi umekamika kwa kiwango cha lami kwa thamani ya sh.bilioni 14,”alibainisha mkuu huyo wa mkoa.
Alisema kutoka Masana kwenda mpaka Mbezi mwisho ambao ni urefu wa kilomita 16 ujenzi umekamilika ambapo kiasi cha sh.bilioni 24 kimetumika .
“Katika eneo la Masana kero kubwa pia ilikuwa ni maji yanayo toka katika eneo hilo na Goba yanatawanyika mitaani na kuleta athari kubwa kwa wananchi. TANROADS inajenga mtaro mita 780 kwa sh.bilioni 2.2 na fedha zimetolewa, mkandarasi yuko kazini na ujenzi utakamilika Oktoba mwaka huu,”alisema Makonda.
Aidha alisema ujenzi wa daraja la kivuko cha watembea kwa mguu katika Barabara ya Bagamoyo eneo la Lugalo uko katika hatua za mwisho na umegharimu sh.bilioni 1.9.
Alieleza, kukamilika kwa barabara ujenzi wa miundombinu hiyo a kutafunguab fursa na kuharakisha maendeleo katika eneo hilo na kwamba huo ni utekelezaji wa ahadi ya serikali bya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli.
Mhandisi Mkazi wa TANROA,) Simon Mganyi, alisema pamoja na kasi kubwa ya ujenzi wa barabara ya Wazo hadi Goba inayojengwa chini ya wakala huo, lakini changamoto iliyopo ni upungufu wa fedha za malipo kwa mkandarasi pamoja na fidia kwa wananchi waliopitiwa na mradi huo.
“Mpaka sasa mkandarasi amelipwa sh.bilioni 1.6 ya kazi yote aliyofanya. Pia Kulipa wananchi wananchi wanadai sh. milioni 200 za fidia. Ujenzi unatarajiwa kukamilika Machi mwakani lakini kama fedha zitatolewa kwa wakati basi tunaweza kukamilisha Desemba mwaka huu kwani muda uliotumika hadi sasa ni asilimia 60,” alieleza Mhandisi Mganyi.
Wananchi katika eneo hilo wamepongeza jitihada za ujenzi wa miundo mbinu hiyo ambapo walisema bmiongoni mwa changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili ni ubovu wa barara uliokuwepo.
Pamoja na hayo Makonda ametembelea Shule ya Sekondari ya Kisauke, Kata ya Wazo hill Wilayani, Kinondoni , jijini Dar es Salaam kushangazwa na kitendo cha wanafunzi na walimu kuchangia choo kimoja.
Kutokana na hali hiyo, walimu wa shule hiyo walilazimika kuuzuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili kuelezea adha hiyo ambayo walisema ni ya muda nrefu.
Hatahiyo Makonda ameahidi kuwajengea vyoo walimu hao ili wasichangia na wanafunzi .
Hivyo makala RC MAKONDA AFUTA AIBU YA WALIMU KUCHANGIA CHOO NA WANAFUNZI,UJENZI BARABARA YA GOBA MBIONI KUKAMILIKA.
yaani makala yote RC MAKONDA AFUTA AIBU YA WALIMU KUCHANGIA CHOO NA WANAFUNZI,UJENZI BARABARA YA GOBA MBIONI KUKAMILIKA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AFUTA AIBU YA WALIMU KUCHANGIA CHOO NA WANAFUNZI,UJENZI BARABARA YA GOBA MBIONI KUKAMILIKA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/rc-makonda-afuta-aibu-ya-walimu.html
0 Response to "RC MAKONDA AFUTA AIBU YA WALIMU KUCHANGIA CHOO NA WANAFUNZI,UJENZI BARABARA YA GOBA MBIONI KUKAMILIKA."
Post a Comment