Loading...
title : Serikali Kutekeleza Miradi Kwa Kushirikiana na Sekta Sekta Binafsi Yenye Thamani ya Mabilioni ya Shilingi.
link : Serikali Kutekeleza Miradi Kwa Kushirikiana na Sekta Sekta Binafsi Yenye Thamani ya Mabilioni ya Shilingi.
Serikali Kutekeleza Miradi Kwa Kushirikiana na Sekta Sekta Binafsi Yenye Thamani ya Mabilioni ya Shilingi.
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuanzisha
na kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa ubia kati
ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) ambapo miradi zaidi ya
11 iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji lengo likiwa
ni kufanikisha azma ya kuwa na uchumi wa viwanda.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Idara ya Ubia Sekta ya
Umma na Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt.
John Mboya wakati akiwasilisha mada ya utekelezaji wa
dhana ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika miradi ya
maendeleo nchini kwenye semina iliyowashirikisha
mawaziri, naibu mawaziri na baadhi ya watendaji wa serikali
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
jijini Dodoma.
Akiwasilisha mada hiyo, Dkt. John Mboya amesisitiza
umuhimu wa kuwepo kwa umakini mkubwa katika uandaaji
na utekelezaji wa dhana hiyo ya ubia Sekta ya Umma na
Binafsi kwa kuzingatia sheria, sera, miongozo, kanuni na
taratibu mbalimbali zilizopo.
Aidha alizitaka taasisi na wadau wa utekelezaji kuwa tayari
kujifunza kutoka katika nchi zilizoendelea kupitia dhana hii
ya ushirikikishwaji wa sekta binafsi katika kuchochea ukuaji
wa viwanda na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Dkt. Mboya aliitaja baadhi ya miradi iliyoko katika hatua
mbalimbali ya utekelezwaji kwa Ubia kati ya Sekta ya Umma
na Binafsi kuwa ni mradi wa mabasi yaendayo haraka
(DART), Ujenzi wa Viwanda vya dawa, mradi wa VETA
utakaohusisha ujenzi wa vyuo 10 ambavyo vinatarajiwa
kutoa ujuzi mbalimbali kwa wanafunzi wapatao 90,000 ili
kukidhi mahitaji ya wataalamu watakao saidia kufanikisha
uchumi wa viwanda.
"MIradi Mingine ni Ujenzi wa Bandari ya Mwambani,
barabara ya Dar es salaam hadi Chalinze, Ujenzi wa Reli
kwenye miradi ya Mchuchuma hadi Mbambabay mikoa ya
Kusini ya Lindi na Mtwara, Ujenzi wa Reli kuanzia Tanga,
Arusha hadi Musoma, na mradi wa umeme wa Chuo Kikuu
cha Dodoma.
Akijibu swali la Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa, Josesph Kakunda, aliyetaka kujua
kuhusu kuondolewa kwa sheria ya utekelezwaji wa miradi
kwa Ushirikishwaji wa Pamoja kati ya serikali na sekta
binafsi (Joint Venture) ambayo haikufanikiwa kama
ilivyokusudiwa hapo awali, Dkt. Mboya alisema kuwa sheria
hiyo haijaondolewa bali miradi hiyo itatekelezwa kupitia
sheria ya Kampuni.
Akichangia katika mjadala wa semina hiyo, Naibu Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya,
alisema ni vema wakati wa kuchagua miradi wahusika wawe
makini ili kuepuka kuanzisha miradi inayofanana na ambayo
inaweza kuwa chanzo cha kufa kwa miradi iliyotangulia.
"Ninashauri kuwepo kwa fursa ya ushirikishwaji katika
miradi midogo ambayo ina manufaa kwa wananchi ikiwemo
ya ujenzi wa nyumba za waalimu" Alisema Mhandisi
Manyanya
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, alizitaka
taasisi ambazo zinatekeleza miradi kwa ubia na sekta binafsi
zielezee umma wa watanzania mafanikio yaliyopatikana ili
kuhamasisha wadau wengine kufuata nyayo hizo
huku akitolea mfano Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini
(TPDC) ambalo nalo liko katika utekelezaji wa dhana hiyo.
Mwenyekiti wa semina hiyo Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alisema kuwa Serikali
imepeleka Muswada Bungeni unaohusu PPP, ambao
ukipitishwa na Bunge linalotarajiwa kuanza Septemba 4,
2018, utekelezaji wa ubia huo utakwenda kwa kasi zaidi ili
kuiwezesha nchi kufikia malengo yake ya kukuza uchumi na
kuleta maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge , Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister
Mhagama, akiahirisha mafunzo hayo, aliwataka wadau wa
semina hiyo kuendelea kukutana na kuelimishana hadi hapo
marekebisho ya sheria hiyo ya Ubia Sekta ya Umma na
Binafsi (PPP) yatakapofanyika.
"Utekelezwaji wa dhana hii ya Ubia Sekta ya Umma na
Binafsi ndio njia rahisi itakayosaidia kukamilisha miradi
mingi ambayo imeainishwa katika ilani ya uchaguzi ya
Chama Cha Mapainduzi (CCM) na kwenye Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, bila ushirikiano huu
na sekta binafsi hatuwezi kufikia uchumi wa viwanda kwa
kasi inayotakiwa’’ Alisema Waziri Mhagama.
Semina hiyo ya siku moja imeendeshwa na wataalamu wa
masuala ya Ubia Sekta ya Umma na Binafsi kutoka Benki ya
Dunia, ambapo Jumapili, kamati tatu za Bunge zitapatiwa
elimu na kujengewa uwezo kuhusu dhana hiyo ya PPP.
Hivyo makala Serikali Kutekeleza Miradi Kwa Kushirikiana na Sekta Sekta Binafsi Yenye Thamani ya Mabilioni ya Shilingi.
yaani makala yote Serikali Kutekeleza Miradi Kwa Kushirikiana na Sekta Sekta Binafsi Yenye Thamani ya Mabilioni ya Shilingi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Kutekeleza Miradi Kwa Kushirikiana na Sekta Sekta Binafsi Yenye Thamani ya Mabilioni ya Shilingi. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/serikali-kutekeleza-miradi-kwa.html
0 Response to "Serikali Kutekeleza Miradi Kwa Kushirikiana na Sekta Sekta Binafsi Yenye Thamani ya Mabilioni ya Shilingi."
Post a Comment