Loading...
title : TANZIA: GWIJI WA MUZIKI WA REGGAE NCHINI JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA
link : TANZIA: GWIJI WA MUZIKI WA REGGAE NCHINI JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA
TANZIA: GWIJI WA MUZIKI WA REGGAE NCHINI JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA
Na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Habari zilizotufikia katika chumba chetu cha habari usiku huu zinasema kwamba gwiji wa muziki wa reggae nchini Jah Kimbute (pichani) amefariki dunia nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam, mshirika wa karibu wa marehemu David Msitta Manju, amethibitisha.

Amesema kwamba amepata taarifa hizo toka kwa mkewe aliyeko jijini Tanga na kwamba mipango ya mazishi itajulikana leo asubuhi baada ya ndugu kukusanyika.
Mke wa marehemu pia alithibitisha habari hizo akiwa Tanga, na kusema kila kitu kitafahamika baada ya ndugu wa Jah Kimbute kukutana.
Amesema marehemu alikuwa akiishi na mwanae nyumbani kwake Msasani na kwamba jana jioni alipokwenda chumbani kwake alimkuta amefariki.
"Hizi habari tumezipata usiku huu na sasa ndugu wa marehemu ambao wengi wako Lushoto wanakusanyika tayari kwa safari ya Dar es salaam kesho kukamimlisha mipango yote.
Jah Kimbute, ambaye jina lake halisi alikuwa Samwel Mleteni, alitamba sana katika anga ya muziki na kuitwa Mfalme wa Reggae wa Tanzania miaka ya 80 akiwa na kundi lake la Roots and Culture lililokuwa na makaazi yake jijini Dar es salaam.
Hivyo makala TANZIA: GWIJI WA MUZIKI WA REGGAE NCHINI JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA
yaani makala yote TANZIA: GWIJI WA MUZIKI WA REGGAE NCHINI JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZIA: GWIJI WA MUZIKI WA REGGAE NCHINI JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/tanzia-gwiji-wa-muziki-wa-reggae-nchini.html
0 Response to "TANZIA: GWIJI WA MUZIKI WA REGGAE NCHINI JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA"
Post a Comment