Loading...
title : Teaba wageukia kuibua mabondia chipukizi
link : Teaba wageukia kuibua mabondia chipukizi
Teaba wageukia kuibua mabondia chipukizi
Na TUZO MAPUNDA
CHAMA cha Ngumi za Ridhaa Temeke (Teaba) kimesema kuwa kina mipango ya kuhakikisha kinawaibua mabondia wapya kupitia mpango wao wa kuanzisha mashindano ya mara kwa mara.
Akizungunza na mwambawahabari.blogspot.com mwenyekiti wa chama hicho, Said Omar ‘Gogopoa’ alisema kuwa kutokana na sababu mbalimbali kwa muda wa miaka miwili hawajafanya mashindano yoyote hivyo wamekosa kupata mabondia wapya.
Alisema kuwa baada ya kuona hivyo chama kimejipanga kikamilifu kuanzisha mashindano ya mara kwa mara ambapo itasaidia kupata mabondia chipukizi na pia kuwaongezea uzoefu wakongwe.
Aliongeza kuwa kwa miaka ya nyuma Temeke imekuwa ikipata heshima kubwa kwa kutoa mabondia waliotikisa nchi lakini kwasasa inaonekana kusuasua hivyo wameona kuna haja ya makusudi kuhakikisha wanarudisha heshima hiyo.
“Sisi kama chama tunataka kuona mabondia wazuri kila siku na kuona mabondia wapya wakijitokeza kila siku, kwa mika miwili hatujafanya mashindano kutokana na kukosa wadhamini na sababu zingine, lakini sasa tumejipanga kuona tunafanikisha tunafanya mashindano mara kwa maram” alisema Gogopoa.
Gogopoa aliendelea kwa kusema kuwa tayari wameshapanga kufanya mashindano ya Klabu Bingwa Mkoa wa Temeke ambapo wanatarajia kufanya Desemba mwaka huu.
Alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha mabondia kutoka klabu zote za Temeke ili kupata timu ya kushiriki mashindano mbalimbali ya kitaifa.
Aliongeza kuwa huu ni muda kwa klabu kuanza maaqndalizi kwa kuwafua mabondia wao ili kuweza kuleta ushindani mkubwa katika mashindano hayo.
Alifafanua kuwa bado hawajawazipa taarifa rasmi klabu lakini mipango itakapokamilika watawataarifu ili waanze maandalizi mara moja.
“Kwasasa tupo kwenye harakati za kufanikisha bonanza letu la kuchangia damu kwa mama wajawazito na watoto ambalo litafanyika mwisho wa mwezi huu, baada ya hapo ndipo tutakaa kuona lini mashindano hayo ya klabu bingwa yatafanyika.
“Tunafikiria tuyafanye Desemba mwaka huu ili mpaka Januari mwakani tuwe tumeshapata timu ya kushiriki katika mashindano ya kitaifa,” alisema Gogopoa.
Hivyo makala Teaba wageukia kuibua mabondia chipukizi
yaani makala yote Teaba wageukia kuibua mabondia chipukizi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Teaba wageukia kuibua mabondia chipukizi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/teaba-wageukia-kuibua-mabondia-chipukizi.html
0 Response to "Teaba wageukia kuibua mabondia chipukizi"
Post a Comment